BIL. 1.5 ZATUMIKA TARIME UJENZI WA SHULE ZA MSINGI NA AWALI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius
Ndejembi amesema kiasi cha Sh Bilioni 1.512 zimepelekwa katika Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na
Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara BOOST.\n\nMhe Ndejembi ameyasema hayo leo
wakati akieleza mafanikio ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwenye ziara ya Waziri Mkuu
Mhe Kassim Majaliwa katika Halmashauri hiyo.\n\nMhe Ndejembi amesema Sh Bilioni
1.08 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mpya za msingi, Sh Milioni
325 zikitolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 13 mapya pamoja na Sh Milioni 69
ambazo zilitolewa kwa ajili ya madarasa ya mfano elimu ya awali.\n\n“ Fedha
hizo siyo kwenye elimu ya msingi tu. Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia
mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari SEQUIP tumeleta fedha Sh
Milioni 470 katika Kata ya Sirari kwenye awamu ya kwanza, awamu ya pili Sh
Milioni 584 kata ya Manga na Sh Milioni 100 kwa ajili ya nyumba ya walimu
Sirari,” Amesema Mhe Ndejembi.
Comments
Post a Comment