KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA CHA NGURU HILLS NA KURIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA PSSSF KWENYE MRADI HUO


NA MWANDISHI MAALUM, MOROGORO.
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Jerry Silaa, imeridhishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)  kwenye Mradi wa Uendelezaji wa shamba (Rachi) ya kunenepesha Mifugo na Machinjio ya kisasa wa Nguru Hills Ranch ulioko Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Kufuatia kuridhishwa huko  Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jerry Silaa alitoa maagizo matatu kwa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF kuhakikisha inaendelea kusimamia mkataba wa uwekezaji katika machinjio hayo ya Nguru Hills kwa kushirikiana na wawekezaji wenza kwa lengo la kuhakikisha uzalishaji unaanza haraka iwezekanavyo na kupata tija iliyokusudiwa.
Pia Bodi ya PSSSF imeagizwa kuongeza kipengele kwenye makubaliano ya ubia na wawekezaji wenza kwenye machinjio hayo ya kukiuzia Ngozi kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro Leather Industry Company Limited (KLIC) ambacho PSSSF imewekeza na hivyo kiwanda cha KLIC kitapata uhakika wa Malighafi na hivyo kupata tija ya uwekezaji huo.
"Kamati pia inaagiza Bodi ya PSSSF kwa kushirikiana na wawekezaji wenza kuanzisha Program Maalum ya Elimu kwa Wafugaji ili kupata mifugo itakayokidhi viwango vinavyohitajika kwenye kiwanda." Alisisitiza.

Katika Mradi huo PSSSF inamiliki asilimia 39 ya hisa, huku wawekezaji wenza Kampuni ya Eclipse Investiment LLC ina hisa asilimia 46 na kampuni ya Busara Investment LLP yenye hisa asilimia 15.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C.P.A Hosea Kashimba  alisema, Mradi upo katika hatua ya majaribio na makabidhiano (testing and commissioning) kabla ya kuanza uzalishaji rasmi.  
Alisema Ukarabati wa jengo la kiwanda pamoja na mifumo ya maji na umeme  umekamilika kwa asilimia 98 na ujenzi unatekelezwa na kampuni ya Help Desk Engineering company limited kwa gharama ya shilingi 3,044,000,000.00.
Aidha ufungaji wa mashine za kuchinjia na mifumo ya kupoozea umekamilika kwa asilimia 98 ambapo Mashine hizo ziliagizwa kutoka China kwa thamani ya dola 1,540,232.00 Mashine zote zimeshafungwa kiwandani na hatua inayofuata ni majaribio na makabidhiano alisema C.P.A Kashimba.
Maeneo mengine ambayo yamekamilika ni pamoja na Ujenzi wa banda la kuhifadhia wanyama kabla ya kuchinjwa, 
Ujenzi wa mabwawa ya kutibu maji taka umekamilika kwa asilimia 100. Ujenzi huu ulihusisha uchimbaji na ujenzi wa mabwawa sita (6) uliofanywa na Kampuni ya Superb Builders – Tanzania kwa gharama ya shilingi 1,066,867,200.00
Kuhusu miundombinu ya barabara Mkurugenzi Mkuu huyo alisema Utengezaji wa barabara yenye urefu wa km 7.2 kwa kiwango cha changarawe kutoka barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Makunganya, kwa sasa imekamiliaka kwa asilimia 100. Ujenzi wa barabara hii uligharimu kiasi cha shilingi 469,559,745.80 na ulisimamiwa na TARURA Wilaya ya Mvomero.
C.P.A Hosea Kashimba alisema, PSSSF imerithi Uwekezaji huo kutoka uliokuwa mfuko wa LAPF ambao uliwekeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 3.9 mnamo.mwak 2017 huku wawekezaji wengine wakiwekeza mtaji wa jumla ya dola za Kimarekani milioni 6.1.
Alisema tathmini ya thamani ya mradi (valuation) iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Ardhi mwaka 2017 ilionesha kwamba thamani ya mradi kwa wakati huo ilikuwa shilingi bilioni 33.49.
Lengo ya Kampuni ya Nguru ni kuuza asilimia 80 ya bidhaa zake nje ya nchi na asilimia 20 katika soko la ndani ya nchi.
Bidhaa zitakazozalishwa zitakuwa za viwango vya kimataifa kwa kufuata taratibu za HACCP (Hazard Analysis and Critical Control Points) na kwa kufuata misingi ya halal.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mhe. Jerry Silaa (watatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C.P.A Hosea Kashimba (wapili kushoto) na wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando (katikati mwenye suti) wakimsikiliza Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Nyama cha Nguru Hills, Bw.Erick Cormack wakati wa ziara ya Kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mhe. Jerry Silaa, akizungumza mara baada ya Kamati yake kutembelea Mradi wa Uendelezaji wa shamba (Rachi) ya kunenepesha mifugo na machinjio ya kisasa wa Nguru Hills Ranch ulioko Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Machi 31, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C.P.A Hosea Kashimba akizungumza mbele ya Kamati





 



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"