PROF. NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA SITA KUENDELEA KUIMARISHA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi kwa kuwa ni haki ya msingi wa kila mfanyakazi nchini. 

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Aprili 28, 2023 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku, mkoani Morogoro.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mazingira salama na yenye afya kazini ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.” 

Amesema Rais Samia amekuwa kinara katika kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa inalindwa kwa kuendelea kuimarisha Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA).

Waziri Ndalichako amewataka OSHA kuendelea kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na  kuwahamasisha waajiri kuweka mifumo sahihi ya usalama na afya katika maeneo yao ya kazi na kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama na afya sehemu za kazi.

Akizungumza awali, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa masuala ya usalama na afya ni mtambuka na yanagusa nyanja zote za kiuchumi, hivyo OSHA imejipanga katika kuhakikisha mfanyakazi nchini wanafanya kazi kwenye mazingira yenye usalama na afya.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Suzanne Ndomba ameeleza kuwa ili mwajiri awe na tija na ufanisi katika mazingira yake ya kazi ni lazima azingatie usalama na afya wa wafanyakazi wake.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini  Nyamhokya, amesema  Serikali, Waajiri na Wafanyakazi wanawajibu wa kuhakikisha sehemu za kazi wakati wote zinakuwa salama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako, akihutubia kwenye kilele cha sherehe hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu, akizungumza kwenye sherehe hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati wa kilele cha Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro leo Aprili 28, 2023.
Prof. Ndalichako akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda.
Watendaji wa Wizara 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Tuzo    Afisa Usalama Mahali pa Kazi (TPA) Bw. Sharifu Selemani Jirani.
TPA ameibuka mshindi wa Tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye Sekta ya Umma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akimkabidhi Tuzo, Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki, Bi. Zaida Mahavu baada ya Mfuko huo kuibuka mshindi wa Taasisi Bora ya Umma ya Hifadhi ya Jamii kwa kuwa na sera zuri za Usalama na Afya mahali pa Kazi. Tuzo hiyo imetokewa wakati wa kilele cha sherehe za Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya  pa Kazi ambayo Kitaifa ilifanyika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"