MKURUGENZI MKUU WA WCF AKUTANA NA WANUFAIKA WA FIDIA
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (katikati)
akisalimiana na Wanufaika wa Fidia inayotolewa na WCF, Bw. Deus Anthony (kulia)
na Bw. Ramadhan Juma kwenye kilele cha siku ya kimataifa ya usalama na afya
mahali pa kazi katika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro Aprili 28, 2023.
Wawili
hao wamepata ulemavu wa kudumu baada ya kuumia kwa nyakati tofauti wakati
wakitekeleza majukumu ya waajiri wao.
Wakati
Bw. Deus Anthony ambaye aliumia wakati akishiriki ujenzi wa barabara kati ya
Iringa-Igawa alikatika mguu na kufaidika na fao la matibabu kutoka WCF hadi
alipopona.
“Nilikatika
mguu wa kushoto wakati nikiwa kazini
mwaka 2017, WCF wamekuwa na mimi katika matibabu hadi kupona na kasha kunipa
mguu w abandia, naweza kutembea bila ya shida yoyote.” Amefafanua , Bw. Anthony.
“Nawashukuru
WCF kwa kuniwezesha kuyamudu maisha, pensheni ninayolipwa kila mwezi kutokana
na ulemavu wangu wa kudumu, nimekuwa
nikidunduliza na hatimaye nimefanikiwa kumiliki bajaji yangu mwenyewe kutokana
na kipato hicho cha kila mwezi.” Alisema na kuongeza…. hivi sasa nafikiria
kukodi shamba ili nilime maaharage huko Mikumi.” Amesema
Mnufaika
mwingine ni Bw. Ramadhan Juma, mfanyakazi kwenye kiwanda kimoja mjini Kibaha,
mkoa wa Pwani.
Yeye
alikatika mkono wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi, na ameelezea jinsi WCF
ilivyomuhudumia tangu anauguza mkono wake hadi kupona.
“Nilikatika
mkono wakati naendesha mashine pale kiwandani, nimetibiwa na kupona na kama
haitoshi nikapatiwa mkono wa bandia na WCF.” Alisema mnufaika huyo.
Alisema
fidia kila mwezi anayolipwa ba WCF imekuwa ikimsaidia katika kuhudumia wazazi
wake lakini pia wadogo zake.
Dkt. Mduma akikaribishwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki, Bi. Zaida Mahavu na Afisa Uhusiano Mkuu Bw. Abdul Njaidi kwenye banda la PSSSF.
Mkurugenzi Mkuu WCF, Dkt. John Mduma (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar alipotembeela banda la NSSF
Mkurugenzi Mkuu WCF, Dkt. John Mduma akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF mbele ya banda la Mfuko huo baada ya kutwaa tuzo
Comments
Post a Comment