NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI-MAJALIWA

 MOROGORO

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei 1, 2023 kitaifa Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri.


Ameyasema hayo leo Jumapili (Aprili 30, 2023)alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan


Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo yanahitaji maboresho.


Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bi. Fatuma Mwasa amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.


Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tumaini Nyamhokya amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na wanamatarajio kuwa mahudhurio yatakuwa makubwa na sherehe hizo kuwa za mafanikio.





 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"