KAMATI YARIDHIA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA BoT KATIKA UTEKELEZAJI WA SERA YA FEDHA
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
KAMATI ya Sera ya Fedha (Monetary Policy Committee) imeridhia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iendelee na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza ongezeko la ukwasi katika uchumi kwa mwezi Novemba na Desemba 2022.
Tamko hilo la Kamati limetolewa kufuatia kikao chake cha Novemba 28, 2022 ambapo ilifanya
tathmini ya utekelezaji wa sera ya fedha na mwenendo wa uchumi na kwa
kuzingatia athari za mtikisiko wa uchumi
duniani
kwenye mfumuko wa bei na shughuli za uchumi.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Brnki Kuu iliyotolewa kwa vyombo vya Habari Novemba 29,
2022 imesema utekelezaji huu wa sera ya fedha unalenga kuhakikisha kuwa mfumuko
wa bei unaendelea kubakia ndani ya lengo na kuwezesha ukuaji wa uchumi nchini.
Taarifa
kamili inapatikana hapo chini.
Comments
Post a Comment