MWENYEKITI WA BODI, SUMA JKT, MEJA JENERALI (MSTAAFU) FARAH ABDI MOHAMMED AIPONGEZA TAASISI HIYO KWA KUZALISHA BIDHAA BORA
NA
KHALFAN SAID, SABASABA
Meja
Jenerali (mstaafu) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Farah
Abdi Mohammed, amesifu ubora wa bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Uzalishaji
Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) wakati alipotembelea Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa ya 46 ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya
Julius Nyerere, maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Juni
29, 2022.
Meja
Jenerali (mstaafu) Farah, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo
linaloendelea kukua kwa kasi, aliyasema hayo wakati alipotembeela banda la Suma
JKT ili kujionea jinsi watendaji wa taasisi hiyo wanavyowahudumia wananchi
wanaofika kwenye banda hilo.
Baadhi
ya shughuli zinazotekelezwa na SUMA JKT ni pamoja na Viwanda, Biashara, Ujenzi
na Uhandisi, Kilimo na Ufugaji.
Baadhi
ya bidhaa zilizowekwa katika maonesho hayo ni pamoja na zitokanazo na mazao ya
misitu kama vile samani za ofisini, shule na nyumbani, asali, vifaa vya kilimo,
bidhaa za ngozi kama vile viatu, mazao ya mifugo kama vile kuku na mayai na
ufugaji wa samaki.
Akiwa
katika banda hilo, Meja Jenerali (mstaafu) Farah, alipokelewa na Mkurugenzi
Msaidizi wa SUMA JKT, anayeshughulikia Operesheni na Utawala, Kanali Shija Lupi
ambaye alimpitisha kwenye maeneo mbalimbali ya shughuli zinazotekelezwa na taasisi
hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa SUMA
JKT, anayeshughulikia Operesheni na Utawala, Kanali Shija Lupi, alisema Shirika
la SUMA JKT litaendelea kushirikiana na
serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inazidi kukua ili nchi izidi kupata
mapato yatokanayo na shughuli za uzalishaji zitokanazo na kilimo.
Alisema SUMAJKTinashiriki katika maonyesho hayo ili kuwapa fursa wananchi na washiriki wengine kwa ujumla wao kuona bidhaa mbalimbali katika sekta za kilimo, ufugaji, viwanda, biashara na huduma.
Comments
Post a Comment