RAIS SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA IDA NAIROBI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaM he. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze Kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na baadhi ya Watanzania waliofika kumpokea Jijini Nairobi baada ya kuwasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Ua mara baada ya kupokelewa na Watanzania Waishio Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"