HUDUMA YAMAJI YAZIDI KUIMARIKA KATAVI
Wataalam
wa sekta ya maji wakikagua mfumo unaochukua maji kutoa ziwa Tanganyika katika
mrdi wa maji wa kijiji cha Karema. Sehemu ya mradi huo imekamilishwa kwa
kuwatumia wataalam wa Wizara ya Maji kupitia utaratibu wa force account.
Mkurugenzi
Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (kushoto),
akimsikiliza Afisa Tarafa wa kijiji cha Karema, wilayani Tanganyika Bw.
Mbonimpaye Mtiyonza Nkoronko, anayeelea kuhusu huduma ya maji katika eneo lake
la kazi, ambapo huduma hiyo inatolewa kwa saa 24, katika vituo 14 vya wananchi,
na baadhi waliounganishiwa katika makazi yao.
Huduma ya maji mkoani Katavi inazidi kuimariki baada
ya miradi ya maji iliyokuwa ikitekelezwa kukamilika na wananchi kuanza kupata
huduma hiyo karibu na makazi yao.
Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa
Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Katavi Mhandisi Peter Mugula amesema kuimarika
huko ni matokeo ya jumla ya miradi ya
maji 14 kukamilika. Ameongeza kuwa miradi 24 ipo katika hatua mbalimbali za
utekelezaji na inatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 2020.
Mhandisi Mugula amesema hadi mwezi Agosti 2020
asilimia 62 kutoka asilimia 51 ya wakazi waishio vijijini tayari walishapata
huduma ya maji, na mjini asilimia ya ilipanda hadi 75 kutoka asilimia 40 ya
wananchi waliokuwa wakipata huduma ya maji. Amefafanua kuwa mabadiliko hayo
yametokana na baadhi ya miradi kukamilishwa na wataalam wa sekta ya maji kwa
utaratibu wa force account.
Ameainisha kuwa miradi ya maji ya mjini inasimamiwa na
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MUWASA), ambapo hivi sasa mamlaka
hiyo imeanza maandalizi ya kujenga mradi wa maji wa Kanoge II utakaozalisha
maji mita mita za ujazo 1,200. Mradi wa Kanoge utaimarisha zaidi upatikanaji wa
maji hadi kufikia mita za ujazo 8,700 hivyo kufanya kiwango cha upatikanaji
maji kufika asilimia 87.
Mhandisi Mugula amesema kuwa lengo ni kuwafikia
wananchi wote katika huduma ya maji na hakuna atakayeachwa. Takwimu za sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa mkoa wa Katavi una jumla ya watu
564, 604 na mwaka 2018 mkoa huo ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu 738, 237.
Comments
Post a Comment