TANZANIA YA TATU KWA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI BARANI AFRIKA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amebainisha kulingana na tafiti za kimataifa Tanzania ni nchi ya tatu kwa Mazingira mazuri ya Uwekezaji barani Afrika, ikitanguliwa na Nigeria na Afrika Kusini.

Amesema hayo leo Oktoba 31, 2023 jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa jukwaa la Biashara lililowakutanisha wawekezaji kutoka Tanzania na Ujerumani.
Aliongeza kuwa maboresho yaliyofanyika katika sheria, sera na kiutumishi chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yamepelekea kufanya vizuri katika Uwekezaji barani Afrika.
Prof. Mkumbo amebainisha kuwa maeneo aliyojadiliana ambayo Ujerumani yanaweza kuwekeza ni pamoja na Nishati jadilifu, kuzalisha umeme wa maji, jua na upepo pia uzalishaji wa madini ya kimkakati ya kutengeneza betri na kuunganisha magari ikiwemo Volkswagen.
" Tunakaka Tanzania kuchukua nafasi yake katika ukanda Afrika katika kuwekeza Viwanda vya kutengeneza magari".
Prof. Mkumbo ameongeza ujumbe huo umetoa pongezi zao kwa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuboresha Mazingira ya Uwekezaji pia wameomba Serikali kuendelea kuboresha masuala nishati na bandari.
Kongamano hilo limejumuisha viongozi wa Serikali pamoja na wawekezaji wa kutoka Ujerumani na Tanzania.
Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini. Kwa mujibu wa TIC hadi kufikia Agosti 2023, Ujerumani imewekeza katika miradi 178 yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 408.11 na kutoa fursa za ajira zipatazo 16,121.
Ilibainishwa kuwa Makampuni ya Ujerumani yamewekeza katika sekta kadhaa za uchumi wa Tanzania kama vile kilimo, ujenzi, taasisi za kifedha, uzalishaji, uchimbaji madini, huduma za usafirishaji, nishati, mawasiliano, utalii na maliasili.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"