NAULI MPYA ZA DALADALA NA MABASI YA MIKOANI KUANZA KUTUMIKA WIKI MBILI ZIJAZO: LATRA

 20220430_133745Mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu (LATRA) imetangaza bei mpya za nauli za mabasi na daladala nchini.

Akitangaza kiwango hicho kipya cha nauli leo Jumamosi Aprili 30, 2022 Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliard Ngewe amesema kiwango hicho kipya kitaanza kutumika baada ya siku 14.
Ngewe amesema nauli mpya ya daladala kuanzia KM 0-10 itakua Tsh. 500 kutoka Tsh. 400 na KM 11-15 nauli itakua Tsh. 550 kutoka Tsh. 450 na bei ya mwisho ya daladala kwa KM 36 hadi 40 itakua Tsh. 1100 kwa daladala tu.
IMG_20220430_133203

Kwa upande wa nauli za mabasi yaendayo mikoani zimepanda kwa daraja la kawaida ni Tsh. 41.29 kwa KM moja kutoka Tsh. 36.89 huku daraja la kati likipanda kwa shilingi 56.88 kutoka Tsh. 53.22.
Nauli kwa wanafunzi imebakia kuwa Tsh. 200 kwa daladala.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"