MCHUNGAJI PETER MSIGWA "AMWAGIA SIFA" RAIS SAMIA, NI KUTOKANA NA FILAMU YA THE ROYAL TOUR

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufuatia juhudi kubwa anazofanya za kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour.

Mchungaji Msigwa ameita kitendo hicho cha Mhe. Rais kuwa ni jambo la kizalendo na anapaswa kutiwa moyo na kila Mtanzania.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa tweeter Mchungaji Msigwa ameendelea kusema kuwa Kwa namna iwayo yote ile hii ni hatua kubwa positive.

“Inawezekana kunaweza kuwa na mapungufu kwenye Filamu ya ROYAL TOUR! Lakini jambo alilolifanya Mh SSH ni jambo la kizalendo na la kutiwa moyo. Mara nyingi nikiwa bungeni nimeshauri kuitangaza Tanzania kwa nguvu kimataifa. Kwa namna iwayo yote ile hii ni hatua kubwa positive.” Ameandika Mchungaji Msigwa.

Tayari filamu ya The Royal Tour imeshazinduliwa nchini Marekani na sasa inaendelea kufanyiwa uzinduzi nchini ambapo Aprili 28, 2022 ilizinduliwa kwenye mji wa kitalii wa Arusha, na kasha itafuatiwa na miji ya Dar es Salaam na Zanzibar lengo kubwa la filamu hiyo ni kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini ambapo Rais ndiye muhusika mkuu kwenye filamu hiyo na amecheza kama Tour Guide

Rais Samia
Mchungaji Peter Msigwa



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"