WATUMIAJI HUDUMA NDOGO ZA FEDHA WAASWA KUTUMIA HUDUMA HIYO KWA TAASISI ZILIZOSAJILIWA
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WATUMIAJI
wa Huduma ndogo za fedha wameaswa kutotumia huduma kwa mtu au taasisi ambayo
haijasajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Msimamizi wa Huduma Ndogo za fedha BoT, Bi. Mary Ngasa
wakati wa majadiliano baada ya kuwasilisha mada “Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha, (Microfinance Supervision)”
kwenye semina ya siku moja kwa Wahariri wa vyombo vya habari kuhusu masuala ya Fedha
na Uchumi iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam Februari
27, 2023.
Alisema
hadi sasa kuna jumla ya taasisi za watoa huduma ndogo za fedha zinazofikia 1,000
ambazo zimesajiliwa na BoT, Tanzania Bara.
Akifafanua
alisema “Ibara ya 12 ya Sheria hiyo imeipa mamlaka Benki Kuu ya Tanzania
Kusajili, Kusimamia na Kudhibiti biashara ya huduma ndogo za Fedha Tanzania
Bara, lengo kuu hasa ni kuwasaidia wananchi kuepuka changamoto za udanganyifu
zilizokuwa zikiwakumba kabla ya kuanzishwa kwa sheria.” Alifafanua
Alisema
Ibara ya 16 ya Sheria hiyo imetoa katazo kwa mtu au taasisi yeyote kufanya
biashara ya kutoa huduma ndogo za fedha bila kuwa na leseni iliyotolewa na
Benki Kuu ya Tanzania inayoruhusu kufanya biashara hiyo.” Alifafanua na
kuongeza
“Tuwe
na mazoea ya kuwafahamu watoa huduma ndogo za fedha kabla ya kufikwa na
matatizo, kuna haki za msingi ambazo mwananchi anapaswa kuzifahamu ili kuepuka
udanganyifu.” Aliasa.
Bi.
Mary Ngasa alisema sheria imetoa tafsiri juu ya “huduma ndogo za fedha” kuwa ni
biashara inayojumuisha kupokea fedha, kama amana au riba kutokana na amana au
mkopo na kuikopesha kwa wanachama au wateja; kupokea amana na kutoa mikopo au
huduma ya mikopo kwa wajasiriamali wadogo, kaya au mtu mmoja mmoja.
Aidha amewataka watoa huduma kufuata maelekezo ya BoT na Kanuni zilizowekwa katika uendeshaji wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na kutoa hati ya mkataba kwa maandishi kwa watumiaji (wateja) wa huduma.
Kaimu Msimamizi wa Huduma Ndogo za fedha BoT, Bi. Mary Ngasa, akiwasilisha mada.Wahariri wakifuatilia uwasilishwaji wa mada.
Comments
Post a Comment