TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. TRIL 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND
Na Farida Ramadhani, WF, Dodoma
Tanzania
na Global Fund zimesaini Mikataba minne ya misaada yenye thamani ya dola za
Marekani milioni 606.9 (sawa na zaidi ya sh. trilioni 1.4) kwa ajili ya
kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo
ya afya nchini.
Mikataba
hiyo imesainiwa Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba Madelu (Mb), na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden Morrison.
Mhe.
Nchemba alisema msaada kutoka Global Fund umepangwa kutekelezwa kwa miaka
mitatu ambapo mpaka sasa Tanzania imepokea misaada kwa vipindi vinne ambavyo ni
Julai 2012 – Desemba 2014, Julai 2015 – Desemba 2017, Januari 2018 – Desemba
2022 na Januari 2021 -Desemba 2023.
“Miradi
inayotekelezwa kupitia msaada wa Global Fund kwa kipindi cha kuanzia Januari
2024 hadi Desemba 2026 itatekelezwa na Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara
ya Fedha inaendelea kuwa Mpokeaji Mkuu wa Sekta ya Umma na Management and
Development for Health (MDH) ni Mpokeaji Mkuu wa pili kwa Sekta Binafsi”,
alibainisha Mhe. Nchemba.
Aidha,
aliishukuru Global Fund kwa kuendelea kuisaidia Tanzania na kubainisha kuwa
misaada hiyo inatokana na juhudi mbalimbali anazofanya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameifanya nchi
iaminike Kimataifa.
Kwa
upande wake Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu alisema watatumia fedha hizo
kikamilifu katika kuimarisha kinga dhidi ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu
ambapo asilimia 75 ya fedha hizo wamezielekeza kwenye bidhaa za afya.
“Kwa
upande wa UKIMWI tutahakikisha takribani Watanzania milioni 1.7 ambao
wanamaambukizi wanapata dawa za kufubaza makali ya UKIMWI au ARV’s kila mwaka”,
alisema Mhe. Mwalimu.
Alisema
kwa upande wa malaria, fedha hizo zitatumika kuiwezesha Wizara hiyo kuendelea
kutoa huduma bure ya kupima Malaria kwakutumia kipimo cha haraka (MRDT) na
kutoa dawa za Malaria kwa watu takribani milioni 10 kwa kipindi cha miaka
mitatu.
“Nasisitiza
kwamba kipimo cha Malaria cha haraka (MRDT) ni bure, dawa mseto ya Malaria
pamoja na sindano ya Malaria kali ni bure kwa sababu fedha hizi tulizopata
kutoka Global Fund tunakwenda kutumia kununua vifaa vya kupima Malaria pamoja
na dawa”, alisisitiza, Mhe. Mwalimu.
Aidha,
aliwaagiza Waganga Wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini kusimamia maelekezo ya
Serikali ya kuhakikisha huduma hizo zinatolewa bure kwa wananchi.
Alisema
katika upande wa Malaria pia watagawa vyandarua vyenye dawa takribani milioni
22.6 kwa makundi mbalimbali hususan akina mama wajawazito na Watoto walio chini
ya miaka mitano.
Kwa
upande wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu, Mhe. Mwalimu alisema watatumia fedha
hizo kwa ajili ya kuhakikisha wanaibua wagonjwa wapya wa ugonjwa huo.
Alisema
fedha hizo pia zitatumika kuimarisha mifumo ya afya ambapo Wizara hiyo imepanga
kununua vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya huduma za afya katika ngazi ya kata.
Naye
Mkuu wa Global Fund Afrika, Bw. Linden Morrison, alisema kuwa Tanzania ni nchi
ya nne kwa kupata misaada mingi kutoka Mfuko huo pia imekuwa mstari wa mbele
katika ukusanyaji na usimamizi wa rasilimali jambo lililosababisha kupewa
misaada hiyo.
Alisema
msaada uliotolewa ni kwa kipindi cha mwaka 2024 hadi 2026 na inalenga kuboresha
mifumo ya maabara, mitungi ya Oksijeni, kuboresha mazingira ya watumishi wa
afya na kuimarisha mnyororo wa thamani.
Aidha Bw. Morrison alisema kuwa msaada huo unakwenda sambamba na vipaumbele vya Serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha mifumo ya Afya nchini.
Ameipongeza
Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha kusimamia utekelezaji wa
programu
iliyoishia Desemba 2023 ambapo ilipata matokeo mazuri ya matumizi ya fedha kutoka
mfuko huo katika masuala yakupunguza maambukizi ya HIV, Maralia na kifua kikuu.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw.
Linden Morrison, wakisaini Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya
takribani dola za Marekani milioni 606.9 (saa na zaidi ya shilingi trilioni
1.4) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na
Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa
Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw.
Linden Morrison wakibadilishana Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya
takribani dola za Marekani milioni 606.9 (zaidi ya shilingi trilioni 1.4) kwa
ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa
mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini
Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameki Nchemba Madelu (Mb), (kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw.
Linden Morrison, wakionesha Hati za Mikataba ya Msaada yenye thamani ya
takribani dola za Marekani milioni 606.9 kwa ajili ya kupambana na maradhi ya
UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameki Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za
Mikataba minne ya Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni
606.9 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4) kutoka Mfuko wa Dunia (Global
Fund) kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na
Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Kambarage, jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu
(Mb) akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za Mikataba minne ya
Msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 (zaidi ya
shilingi trilioni 1.4), uliotolewa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa ajili ya
kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji wa mifumo
ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.
Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw.
Linden Morrison, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Hati za Mikataba
minne ya msaada yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 606.9 (sawa
na zaidi ya shilingi trilioni 1.4), uliotolewa na Mfuko wa Dunia (Global Fund)
kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na
Uimarishaji wa mifumo ya afya nchini, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa
Kambarage, jijini Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Management and Development for Health
(MDH), Dkt. David Sando(kushoto) na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Bw. Linden
Morrison, wakionesha Hati za Mkataba wa masaada wa mapambano dhidi ya UKIMWI NA
Kifua Kikuu katika hafla ya utiaji saini Mikataba ya Msaada wenye thamani ya
takribani Dola za Marekani milioni 606.9 uliotolewa na Global Fund kwa ajili ya
uimarishaji wa mifumo ya afya nchini ikiwemo kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu
pamoja na Malaria, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kambarage, jijini
Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Comments
Post a Comment