AFRIKA TUMIENI VEMA FURSA ZA SOKO LA AFCFTA

 Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afika (AfCFTA) amezisitiza Nchi Wanachama wa Mkataba huo kutumia vema fursa zilizopo ili kukuza biashara.


Dkt. Kijaji ameyasema hayo Januari 30, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024.

Aidha amezitaka Nchi hizo kuendelea kushirikiana katika kukamilisha Itifaki ya Uwekezaji, Itifaki ya Biashara ya Kidigitali, pamoja na majadiliano kwenye Vigezo vya Uasili wa Bidhaa na kukamilisha masuala muhimu yanayohusu mifumo ya utatuzi wa migogoro katika ufanyaji biashara kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara.

Akifafanua zaidi, Dkt Kijaji amesema ushirikiano wa nchi hizo kupitia AfCFTA utachangia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya usafirishaji wa barabara, reli na usafiri wa anga, usalama, ukosefu wa nishati ya kutosha, uzalishaji mdogo na mawasiliano.

Mkutano huo wa 13 wa Mawaziri ulitanguliwa na mikutano kadhaa katika ngazi ya Wataalam ikiwemo Mkutano wa 16 wa Kamati ya Makatibu Wakuu pamoja na mkutano wa 10 wa masuala ya Kamati ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara iliyofanyika Januari 23 hadi 29, 2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) (kulia) Januari 30, 2024 akifungua   Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024 ambapo Tanzania,  ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AfCFTA kwa mwaka huu 2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa AfCFTA Mhe. Wamkele Mene  baada ya kufungua Mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 30 hadi 31 Januari 2024 ambapo Tanzania,  ni Mwenyekiti wa Mikutano ya AfCFTA kwa mwaka huu 2024.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"