SHAKA AWASHA RASMI MTAMBO WA KUSAMBAZA MAJI PAMOJA NA KUSHIRIKI UJENZI WA SHULE MAALUM YA SEKONDARI YA WASICHANA .

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, leo amewasha mtambo wa maji na tone la kwanza la maji likatoka kwa wakazi wa eneo Mitwero mkoani Lindi .

Akizungumza baada ya kuwasha mtambo huo, Shaka alisema kukamilika kwa mradi huo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 na jitihada za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kufikisha huduma za kijanii kwa wananchi.
Mbali na mradi huo, pia shaka ametembelea na kushiri ujenzi wa Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Lindi inayojengwa katika Kata ya Kilangala, Manispaa ya Lindi.
Akizungumza kuhusu ujenzi wa Shule hiyo, shaka amewataka wananchi kuungana katika kupiga vita mambo yote yanayodhalilisha na kukatisha mdoto za mtoto wa kike kupata elimu.
"Nichukue fursa hii kumpongeza Rais Samia kwanza kwa namna ambavyo amekuwa kinara wa usawa wa kijinsia nchini. Tangu ameingia madarakani moja ya jambo ambalo amejipambanua nalo na lazima tukiri hatukuwa vizuri katika kusimamia suala la usawa wa kijinsia, lakini ametoa kipaumbele kwenye jambo hili," amesema.
Pia, Shaka ametembelea mradi wa wanufaika wa fedha za kusaidia kaya masikini zinazosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wa kilimo cha minazi katika Kijiji hicho.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake wa Kijiji hicho, ambao wanajihusisha na mradi wa kilimo Cha mazao mbalimbali ya biashara ikiwemo minazi, Dalini Makwaya, amesema wanatoa shukrani kwa Rais Samia kwa uamuzi wake wa kutoa fedha hizo na kuwafikia moja kwa moja wahusika na hivyo kubadilisha maisha yao.
Aidha, ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, ambapo amepongeza ujenzi wake kutekelezwa kwa kasi na kutaka ukamilike kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika.





Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"