PSSSF KUWEKEZA ZAIDI KWENYE TEHAMA, RASILIMALI WATU ILI KUONEGZA UBORA WA UTOAJI HUDUMA
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM
KATIKA kuhakikisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF) unaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake, sasa
unaelekeza nguvu zake katika matumizi ya TEHAMA na kuendeleza rasilimali watu
ili kuongeza ubunifu na ufanisi, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba,
amesema.
CPA. Kashimba ameyasema hayo kwenye kikao kazi baina
ya Mfuko, Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) na Wahariri wa vyombo vya habari, wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko tangu kuanzishwa kwake Agosti, 2018 hadi Agosti, 2023, kwenye Makao Makuu ndogo ya PSSSF, jengo la Golden Jubilee
Tower, jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2023,
“Kama kuna namna ya kuufanya
Mfuko uwe wa kisasa zaidi basi hayo ndiyo matamanio yetu na tumeanza, lengo
ni kuifanya taasisi iwe rafiki zaidi kwa wanachama wake na yenye miundombinu ya
kutoa huduma bora zaidi bila ya usumbufu wowote.” Alisema.
Alisema kwa
sasa Mfuko unatumia
TEHAMA kwa zaidi ya asilimia 90 katika kazi zake zote na inategemea kufika
asilimia 100 ifikapo Juni, 2024;
“Mifumo hii ni matokeo ya
uwekezaji na uvumbuzi wa Mfuko katika Mifumo kwa kutumia wataalamu wetu wa
ndani ili kuboresha huduma kwa wateja na pia kuimarisha usalama katika kutunza
nyaraka, kufanya malipo na kupokea malipo mbalimbali na matumizi mengine.”
Alifafanua CPA. Kashimba
Alisema kupitia maboresho yaliyofanywa na Mfuko, Mwajiri
anaweza kutengeneza ankara na kulipa michango moja kwa moja akiwa ofisini kwake
bila kuhitaji msaada wa mtu.
“Wanachama pia wanaweza kupata taarifa zao kupitia
simu za kiganjani, wastaafu na wategemezi wanaweza kujihakiki kwa kutumia alama
za vidole (biometric) na tumeenda mbali zaidi, hata mwanachama akiwa nyumbani
kwake anaweza kutumia simu janja (smart phone) kupitia App ya PSSSF kiganjani na
akajihakiki.” Alifafanua.
Kuhusu hali ya Mfuko, CPA Kashimba aliwaambia
Wahariri kuwa, thamani ya Mfuko wa PSSSF, imefikia shilingi trilioni 8.07 katika
kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake huku thamani ya uwekezaji
ikifikia kiasi cha shilingi trilioni
7.92.
Akifafanua kuhsuu uwekezaji alisema unahusisha Hati
fungani za Serikali (60% chini ya kikomo cha 100%), Uwekezaji katika Majengo (15%
chini ya kikomo cha 30%; kiwango cha upangishaji huu ni 100% kwa majengo ya
makazi na 72% kwa majengo ya kupangisha kwa ajili ya ofisi huku matarajioni yakiwa
ni kufika asilimia 80% mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.
Maeneo mengine ya uwekezaji ni Hisa za Makampuni
(12% chini ya kikomo cha 20%), Amana za Mabenki (7% chini ya kikomo cha 35%);
na Maeneo mengine (6%).
Aidha, kuhusu uandikishaji Wanachama na ulipaji wa
Mafao alisema hadi kufikia Juni 2023, idadi ya wanachama wa PSSSF ni 731,183 na
umetumia kiasi cha shiling trilioni 8.88 kulipa mafao kwa wanufaika 262,095, huku
ukilipa pensheni ya kila mwezi shilingi bilioni 67 kwa wanufaika 164,828 na
pensheni hulipwa tarehe 25 ya mwezi husika bila kuchelewa na sasa Mfuko unalipa
Mafao ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,
(TEF), Bw. Deodatus Balile, aliwashukuru waandaaji wa kikao hicho kwani kimetoa
fursa kwa Wahariri kujifunza mengi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.
Vyombo vya habari ndio njia pekee ya kuwafikia
wananchi kwa uhalisia.” Alisema.
Comments
Post a Comment