WANAOPINGA UWEKEZAJI WA DP WORLD KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM NI MAADUI WA MAENDELEO NCHINI

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akizungumza  wakati wa dua maalumu iliyofanywa na waumini dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu iliyodhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akizungumza  wakati wa dua maalumu iliyofanywa na waumini dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu iliyodhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza wakati wa dua hiyo maalumu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba katika akiwa kwenye dua hiyo wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman
Waumini wa dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta wakimsikiliza Mwenmyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman mara baada ya kumalizika Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu
Na Oscar Assenga, TANGA
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kwamba watu wanaopinga uwekezaji wa Kampuni ya DP World katika Bandari ya Dar es Salaam  ni maadui wakubwa wa maendeleo ya watanzania hivyo wanatakiwa kupuuzwa.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman wakati wa dua maalumu iliyofanywa na waumini dini ya Kiislamu katika Taasisi ya Tamta iliyodhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.
Aliisema kwamba siri za uadui huo wanazo wenyewe na waliyoyatamka ni sehemu ya uadui wao hivyo wao kama viongozi wa dini ni wajibu wao kuendelea kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu kila mmoja kwa wakati wake mpaka maadui wote waweze kuteketea.
Aidha alisema lengo la Rais ni nzuri katika kuisaidia nchi hivyo hizo kelele wanazozisikia kila kona ni za maadui kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar ambako viongozi wenyewe pia hufafanua kwamba hakuna Bandari inayouzwa na uwekezaji haufanyika kwenye Bandari zote.
Mwenyekiti huyo alisema uwekezaji huo unafanyika sehemu tu na awali pia waliokuwepo wazungu wa kampuni ya TICTS walifanya shughuli zao kwa muda wa miaka 22 lakini viongozi wa ngazi za juu ikiwemo Rais, Makamu, Waziri Mkuu na wengine waliona hapana lazima kufanyike uwekezaji mkubwa kwenye Bandari.
Alisema uwekezaji huo unafanyika ili ziweze kupatikana fedha nyingi za kuendesha nchi kama alivyofanya TICTs ndio wanakuja kuyafanya DP World isipokuwa wao wanakuja kuboresha zaidi ili manufaa yapatikane hivyo tatizo lipo wapi huo ni aadui ni mkubwa kwa Rais kwa watu wachache.
Mwenyekiti huyo alisema ila watanzania wengi humuombea Rais ili aweze kutimiza lengo la kusaidia nchi ili kila mtu aishi kwa amani na hivyo kupata maendeleo makubwa katika maendeleo nchini ikiwemo barabara mzuri,dawa pamoja na huduma nyengine za msingi.
“Nimefarijika sana kwa mwaliko huo tulioupata kwenye dua maalumu ya kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu na tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke mbali na mahasidi na maadui wasioitakia mema nchi yetu”Alisema
Alisema kwamba uongozi ni dhamana kubwa sana wanaona rais juhudi kubwa kuisaidia jamii waislamu na wasio wasilamu hivyo ni wajibu wetu sote kumuombea dua kweli kweli wao waislamu wajitahidi kumombea Rais na wanafahamu lengo lake ni nzuri.
Hata hivyo alisema lakini wapo watu ambao wamethubutu wanadiriki kumbagua kwa sababu katokea visiwani lakini hawajui huko ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais yupo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania,
Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alisema kwamba wanamuombea Rais Samia kutokana na juhudi kubwa anazofanya za kimaendeleo hapa nchini.
Alisema kwamba mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo inamatumkizi ya dawa za kulevya hivyo katika majumba yetu hakuna mtu hata mmoja ambaye hajaathiriwa na dawa za kulevya kama sio ndugu itakuwa ni jamaa au rafiki.
Mkuu huyo wa mkoa alisema mapambano ya madawa ya kulevya wataendelea nayo kuhakikisha yanakoma na mkoa huo hauendelei kuwa na historia ya dawa hizo kupita mkoani hapa.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"