RC CHALAMILA ATOA WIKI MOJA KWA WAFANYABIASHARA MWENGE WALIOTELEKEZA VIBANDA KURUDI MARA MOJA.
Ni kufuatia wafanyabiashara hao kuondoka eneo
walilopangwa na kuhamishia biashara Barabarani.
Amuelekeza
Mkandarasi anaejenga Majengo ya kituo Cha Afya Kinondoni kuzingatia ubora.
Apongeza Halmashauri ya Kinondoni kwa kubuni mradi
wa Stendi ya Mwenge na Uwanja wa Mpira.
Ampongeza Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kutoa
bilioni 1.5 kwaajili ya Maboresho ya Elimu program ya Boost.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe, Albert Chalamila
ametoa muda wa wiki Moja kwa Wafanyabiashara wa Soko la Mwenge Coca cola
walioacha vibanda vyao na kurudi kupanga biashara Barabarani kurudi kwenye eneo
walilopangwa mara Moja.
RC Chalamila ametoa maelekezo hayo wakati wa Ziara
ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilaya ya Kinondoni
Akikagua mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Mabasi Mwenge
RC Chalamila amepokea malalamiko ya Wafanyabiashara waliosema kitendo Cha
wafanyabiashara kupanga bidhaa chini imepekea kukosekana kwa wateja na kusababisha
mitaji ya biashara kufa.
Kutokana na Hilo RC Chalamila ameelekeza Jeshi la
polisi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kinondoni kuratibu zoezi la
kuhakikisha wafanyabiashara wanarudi kwenye eneo walilopangwa.
Aidha RC Chalamila ameipongeza Halmashauri ya
Kinondoni kwa kubuni mradi wa Stendi ya Mabasi Mwenge na Ujenzi wa Uwanja wa
Mpira kwaajili ya timu ya KMC kwakuwa kukamilika kwake Itasaidia ongezeko la
Mapato kwa Halmashauri.
Ili kuhakikisha uwekezaji huo unakuwa na tija RC
Chalamila ameelekeza Halmashauri hiyo kuzingatia uwazi kwenye mchakato mzima wa
utoaji wa frem za maduka, uwiano mzuri wa gharama ya kupanga ambapo pia
ameshauri maduka ya jumla kuwekwa kwenye gorofa za juu na wale wafanyabiashara
za rejareja kupangwa maduka ya chini.
Pamoja na hayo RC Chalamila ametembelea ujenzi wa
jengo la gorofa Moja kwenye kituo Cha Afya Kinondoni ambapo panajengwa jengo la
Wazazi, jengo la upasuaji na jengo la kulaza wagonjwa wa nje ambapo
amemuelekeza Mkandarasi kutoka kampuni ya Gemini Engineering Construction ltd
kuhakikisha ujenzi unazingatia ubora kwa mujibu wa mkataba.
Hata hivyo RC Chalamila ametembelea na kuzindua
ujenzi wa miundombinu kwenye shule ya msingi Kundichi ambapo amempongeza Rais
Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 kupitia
programu ya Boost inayolenga kuboresha mazingira ya elimu ambapo miongoni mwa
shule zilizonufaika ni shule ya msingi Kundichi, Kisauke, Mapinduzi, Mchangani,
Mkwawa, Mtambani a Shule ya Ali Hassan Mwinyi.
Comments
Post a Comment