RAIS DKT. MWINYI AMEZIKARIBISHA KAMPUNI ZAIDI ZA CHINA KUWEKEZA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA

Changsha, Hunan China

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi amezikaribisha kampuni nyingi za China kuwekeza Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla, kwani kuna ardhi ya kutosha, nguvu kazi nyingi na Afrika ina uthubutu wa kufanya biashara.
Dkt. Mwinyi aliyasema hayo  wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa Biashara kati ya China na Afrika, uliofanyika katika jiji la Changsha jimbo la Hunan China.
Dkt. Mwinyi alisifu ushirikiano baina ya China na Tanzania ambao sasa umetimiza miaka 60 na akaonesha matumaini yake ushirikiano huo utazidi kukua na kuimarika.
Amesema katika miaka miwili iliyopia Afrika imeshuhudia ushirikiano mkubwa na China ambapo biashara imeongezeka kwa zaidi ya dola bilioni 74.
Amefurahi kuona wawekezaji wakubwa wa China wamehudhuria mkutano huo na akabainisha hiyo ni fursa kwa Afrika kujitutumua zaidi na kukaribisha wawekezaji hao barani humo.
Mapema akifungua mkutano huo kwa niaba ya Afrika Rais wa Malawi Lazaro Chikwera ametaka kuwe na mbinu madhubuti za kuzuia jaribio lolote la kupunguza kazi ya ushirikiano baina ya China na Afrika.
Amesema China na Afrika hazina tena muda wa kuzorotesha uhusiano huo na kuwataka Waafrika kutumia kwa vitendo yale yote waliyojifunza kwa muda wote wa ushirikiano na China.
DK.Chakwera amewataka Waafrika kutumia kipindi hiki kutangaza zaidi bidhaa zake mbalimbali.
Ameitaka China kufikiria kuanza kusamehe mikopo yake kwa Afrika hali itakayosaidia bara hilo kuendelea kupiga hatua za maendeleo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya ukumbi wa Mkutano wa Xiangjiang Jiji la Changsha Jimbo la Hunan China kuhudhuria ufunguzi  wa Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Biashara Kati ya China Afrika uliofanyika katika ukumbi huo leo 29-6-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Afrika uliofanyika leo 29-6-2023 katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Viongozi wa Serikali (kulia kwake) Waziri wa Biashara na Viwanda Tanzania Mhe.Ashatu Kijaji, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaban na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Tanzania Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika mkutano huo wa ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China leo 29-6-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea moja ya banda la Maonesho la Kampuni ya China, baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Afrika, uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Han Zheng leo 29-6-2023 katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakitembelea Banda la Maonesho la Tanzania, katika maonesho ya Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Afrika, yaliyofunguliwa leo 29-6-2023 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Han Zheng, katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Biashara na Viwanda Tanzania Mhe.Ashatu Kijaji na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban, wakielekea katika maonesho ya Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Afrika, baada ya ufunguzi wa maonesho hayo uliofanyika leo 29-6-2023 katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Biashara na Viwanda Tanzania Mhe.Ashatu Kijaji na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban, wakielekea katika maonesho ya Ushirikiano wa Biashara Kati ya China na Afrika, baada ya ufunguzi wa maonesho hayo uliofanyika leo 29-6-2023 katika ukumbi wa Xiangjiang Jimbo la Hunan China.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika viwanja vya ukumbi wa Mkutano wa Xiangjiang Jiji la Changsha Jimbo la Hunan China kuhudhuria ufunguzi  wa Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Biashara Kati ya China Afrika uliofanyika katika ukumbi huo leo 29-6-2023.(Picha na Ikulu)

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"