BENKI YA CRDB YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 36.1 KWA SERIKALI
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) wakikabidhi mfano wa hundi kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba (katikati) ikiwa ni sehemu Gawio la Serikali lililotolewa na Benki ya CRDB, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma leo Juni 29, 2022. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais - Tamisemi, David Silinde (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana, Patrobas Katambi (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru. Dodoma, 29 Juni, 2022 - Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amepokea gawio la shilingi bilioni 36.1 linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya Benki ya CRDB kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay. Makabidhiano hayo ya hundi kifani yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Wazi