RAIS SAMIA ATEUA MKUU MPYA WA MAJESHI
NA MWANDISHI WETU
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda(pichani juu) kuwa Jenerali, kisha kumteua
kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).
Kabla
ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu
ya Jeshi (Chief of Operations and Training) na anachukua nafasi ya Jenerali
Venance Salvatory Mabeyo ambaye amestaafu kwa mujibu wa sharia.
Rais
Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni
Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (Chief of Staff – CofS).
Kabla
ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo
Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Vile
vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla
ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ).
Uapisho
wa viongozi hao wa juu wa jeshi utafanyika Alhamisi Juni 30, 2022 Ikulu, jijini
Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment