PSSSF YAWAKARIBISHA WANACHAMA NA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO MAONESHO YA SABASABA
NA MWANDISHI WETU, SABASABA
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewaalika wanachama wake na wananchi kwa ujumla kutembeela banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyoanza Juni 28, 2022 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa.
Afisa Uhusuano Mwandamizi wa PSSSF, Bi. Fatma Elhady amesema imekuwa ni fursa nzuri kwa Mfuko kushiriki katika Maonesho hayo ili kuwawezesha Wanachama na wananchi kwa ujumla kupata taarifa za huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.
“Tunawakaribisha sana Wanachama wetu na wananchi kutembelea Banda namba 13 la Ushirikiano lililoko mtaa wa Mabalozi.” Alisema.
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni "Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji."
Comments
Post a Comment