PSSSF YAPOKEA GAWIO LA BILIONI 11.85 KUTOKA CRDB KWENYE UWEKEZAJI WA HISA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekabidhi gawio lenye thamani ya  Shilingi bilioni 11.85 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF CPA Hosea Kashimba kwa niaba ya Mfuko, kwenye hafla fupi iliyofanyika leo  jijini Dodoma.

Akikabidhi hundi hiyo Mhe. Mchemba  amesema, "nimefurahishwa pia kuona taasisi na mashirika mbalimbali ya Serikali, Halmashauri, pamoja na vyama vya ushirika wanapokea gawio la jumla ya Shilingi bilioni 16.4. Hii inafanya jumla kuu ya gawio tunalolipokea leo kuwa Shilingi bilioni 36.1. Ni jambo la kujivunia sana kwa Benki yetu ya kizalendo".


Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba
Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi (wakwanza kushoto) akiungana na maafisa wengine kwenye hafla ya kupokea gawio kutoka benki ya CRDB jijini Dodoma Juni 29, 2022.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"