MAONESHO YA 46 YA SABASABA 2022: NSSF YAWAKARIBISHA WANACHAMA NA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA NAMBA 13 WAPATE HUDUMA

 NA MWANDISHI WETU, SABASABA

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF) unashiriki katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kuwakaribisha wanachama wake na wananchi kutembelea banda la Ushirikiano namba 13 la Mfuko huo lililoko mtaa wa Mabalozi.


 Maonesho hayo yametoa fursa nzuri kwa Mfuko kukutana na wananchama wake ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Umma, amesema Aisha Sango, Afisa Uhusiano Mwandamizi, NSSF.

"Sisi NSSF tunasema Tunajenga Maisha Yako ya Sasa na Baadaye" karibu tukuhudumie, alisema Bi. Sango.

Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2022 yamebeba kaulimbiu isemayo “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji.”

Afisa Uhusiano Mwandamizi, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Sebera Fulgence, (kulia), na maafisa wengine wa Mfuko huo, wakiwahudumia wananchama waliotembelea banda la Ushirikiano namba 13 la Mfuko huo Juni 29, 2022.

Afisa Matekelezo Mkuu, NSSF, Bi. Asha Salum (kushoto), akimsikliza mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la NSSF ili kuhudumiwa Juni 29, 2022.
Afisa Matekelezo Mwandamizi, NSSF, Bi. Ummy Kimario (kushoto), akimpatia kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za Mfuko, mwananchi  aliyetembelea banda la NSSF ili kupata elimu ya Hifadhi ya Jamii Juni 29, 2022.
Mwananchi huyu aliyetembelea banda la NSSF kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba, akisoma kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za NSSF.
Afisa Matekelezo Mwandamizi, NSSF, Bw.Deogratius Chawinga (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la NSSF ili kupata huduma Juni 29, 2022.
Afisa Matekelezo Mwandamizi, NSSF, Bw.Deogratius Chawinga (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la NSSF ili kupata huduma Juni 29, 2022.
Afisa Matekelezo Mwandamizi, NSSF, Bw.Deogratius Chawinga (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda la NSSF ili kupata huduma Juni 29, 2022.
Afisa Uhusiano Mwandamizi, NSSF, Bi. Aisha Sango (kulia), akimsikiliza Mwnachama huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko ili kupata huduma.



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"