JKCI KUPIMA MAGONJWA YA MOYO, CHANJO YA UVIKO-19 MAONESHO YA SABASABA 2022

 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28/06/2022 hadi tarehe 13/07/2022.

Katika maonesho haya JKCI inafanya upimaji wa afya ya moyo kwa watoto na watu wazima. Pia inatoa chanjo ya UVIKO-19 kama kinga ya ugonjwa huu pamoja na kufanya kipimo cha kuchunguza UVIKO -19 (rapid test) kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo katika njia ya kupumulia.

Taasisi hiyo pia ina wataalamu wa lishe ambao wanatoa elimu ya lishe bora ambayo inawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo na kisukari ambayo ni magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu wa lishe.

 

Kwa wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hii ikiwa ni pamoja na kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

Madaktari mabingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI  ya kina Peter Kisenge, Tulizo Shem, Tatizo Waane, Baraka Ndelwa na Pedro Pallangyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo katika banda letu kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Nyote mnakaribishwa.


Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"