Posts

DOTTO BITEKO ATEULIWA NAIBU WAZIRI MKUU

Image
Mhe. Dotto Biteko

SERIKALI KUENDELEA KULINDA THAMANI YA SHILINGI

Image
  NA FARIDA RAMADHANI, WF, DODOMA Serikali imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kulinda thamani ya shilingi ya Tanzania ikiwemo kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji kutoka nje. Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbogwe, Mhe. Nicodemas Maganga, aliyetaka kujua mikakati ya Serikali kuongeza thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na nchi jirani za Afrika Mashariki. Mhe. Nchemba alisema Serikali inaendelea kulinda thamani ya shilingi nchini ikiwa ni pamoja na shughulikia tatizo la upungufu wa dola ili kuweza kukabiliana na changamoto inayoendelea kutokea duniani. Alisema miongoni mwa hatua zinachukuliwa na Serikali ni pamoja na kushirikisha Sekta Binafsi katika kuimarisha mikakati ya kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi pamoja na kuhimiza wananchi kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini ili kupunguza mah

WAZIRI NCHEMBA AKUTANA NA MKUU WA MAHUSIANO YA KIMATAIFA WA HEINEKEN

Image
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Uhusiano wa kimataifa wa Kampuni inayozalisha kinywaji cha Heineken (Heineken Beverage International) Bw. Frank Ford, kuhusu masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo, nchini Tanzania. Bw. Ford aliambatana na Mkuu na Menaja Mauzo wa Kampuni hiyo nchini Tanzania, Bi. Fatma Mnaro, ofisi za Hazina (Treasury Square) jijini Dodoma.  

RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI KIZIMKAZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi (hawaonekani pichani) mara baada ya kuzindua mradi wa Maji wa Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar. Taswira ya Mradi wa Maji Kizimkazi kama unavyoonekana pichani mara baada ya uzinduzi tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Maji mara baada ya kuzindua mradi wa Maji Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji Kizimkazi katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi .

RAIS SAMIA AIZINDUA HOTELI YA KITALII KWANZA HUKO KIZIMKAZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mmiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza, Bw. Hossam Elshaer wakati alipokuwa akitembelea Hoteli hiyo mara baada ya kuwasili Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na mmiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza Bw. Hossam Elshaer kuashiria ufunguzi wa Hoteli hiyo iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hoteli iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, wageni mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Hoteli iitwayo Kwanza mara baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Ku

KATAMBI: TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA KANUNI ZA MAFAO

Image
  Na Mwandishi Wetu, DODOMA SERIKALI imeendelea kutoa elimu ya kanuni mpya ya mafao ya pensheni (kikokotoo) na hadi Juni 30, mwaka huu wanachama wa mifuko ya pensheni 131,497 na waajiri 5,580 wamefikiwa na elimu hiyo. Adha, Elimu hiyo imetolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amebainisha hayo bungeni Agosti 29, 2023 alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Mhe. Priscus Tarimo aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhusu malalamiko ya wastaafu juu ya kikokotoo kinachotumika kupiga mahesabu na kulipa mafao. Mhe. Katambi amesema mpango wa serikali ni kuendelea kuwaelimisha wananchi hususani waajiri na wanachama wa mifuko hiyo wakiwamo wastaafu kuhusu faida ya kanuni hizo. Amesema kwasasa kwenye mkupuo wa malipo wanufaika asilimia 81

WAZIRI NDALICHAKO NA KATAMBI WAPONGEZWA KWA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA WASTAAFU

Image
  Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi kwa kushughulikia kwa karibu masuala ya wastaafu. Dkt.Tulia ametoa pongezi hizo Agosti 29, 2023 bungeni baada ya Naibu Waziri Katambi kujibu maswali ya wabunge kuhusu masuala ya wastaafu. Amesema “Naibu Waziri ameonesha utayari kama Mbunge ana changamoto apelekewe, mimi ni shahidi wanafanya kazi nzuri Waziri Ndalichako na Naibu Waziri Katambi, wanasikiliza hoja ukiwapelekea na wanafuatilia kuhakikisha mtumishi au mstaafu anasaidiwa.” Amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii huku akipongeza maboresho yanayoendelea kufanywa kwenye utoaji huduma kwa wastaafu. Awali, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imekuwa ikishughulikia masuala ya wastaafu kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye

MKOA WA PWANI WAONGOZA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE KITAIFA

Image
 NA MWANDISHI WETU, PWANI MKOA wa Pwani umetunukiwa tuzo baada ya kuibuka kinara katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2022/23. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Angela Kairuki ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaji SAboubakar Kunenge. Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa - (OR - TAMISEMI) zimeeleza kuwa Mkoa huo umefuatiwa na Lindi katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa mkoa wa Iringa. Kwa upande wa nafasi za Halmashauri, Mkoa wa Pwani umefanikiwa kuingiza halmashauri za Kibaha TC na Kibaha DC katika nafasi kumi za mwanzo. Kibaha TC imekuwa ya na Kibaha DC ikiwa ni ya 10 huku hamashauri zingine za mkoa huo zikiwa zimeshika nafasi juu ya 100 za mwanzo. Halamshauri hizo na nafasi zao kitaifa kwenye mabano ni Kisarawe (17), Rufiji (25), Bagamoyo (26) na Kibiti (54). Zingine ni Chalinze (59), Mafia (91) na Mkuranga (93). Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Angela Kairuki, a

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO AGOSTI 30, 2023

Image