MKOA WA PWANI WAONGOZA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE KITAIFA

 NA MWANDISHI WETU, PWANI

MKOA wa Pwani umetunukiwa tuzo baada ya kuibuka kinara katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka 2022/23.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Angela Kairuki ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaji SAboubakar Kunenge.

Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa - (OR - TAMISEMI) zimeeleza kuwa Mkoa huo umefuatiwa na Lindi katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa mkoa wa Iringa.

Kwa upande wa nafasi za Halmashauri, Mkoa wa Pwani umefanikiwa kuingiza halmashauri za Kibaha TC na Kibaha DC katika nafasi kumi za mwanzo.

Kibaha TC imekuwa ya na Kibaha DC ikiwa ni ya 10 huku hamashauri zingine za mkoa huo zikiwa zimeshika nafasi juu ya 100 za mwanzo.

Halamshauri hizo na nafasi zao kitaifa kwenye mabano ni Kisarawe (17), Rufiji (25), Bagamoyo (26) na Kibiti (54). Zingine ni Chalinze (59), Mafia (91) na Mkuranga (93).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Angela Kairuki, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaji Aboubakar Kunenge (wapili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Rashid Kassim Mchatta, tuzo ya Ubora katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe mwaka 2022.23


Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"