Posts

CCM WANA JAMBO LAO UWANJA WA JAMHURI JIJINI DODOMA LEO.

Image
NA SAID MWISHEHE,MICHUZI TV CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimesema kesho Agosti 29 mwaka huu wa 2020 wana jambo lao ambalo ni la uzinduzi rasmi wa Kampeni za Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dk.John Magufuli huku kikieleza kitatumia nafasi hiyo kuielezea Afrika na Dunia mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ga Tano. Akizungumza leo Agosti 28,2020, katika Uwanja Jamhuri jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amefafanua maandalizi yote kuelekea uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais na ratiba itaanza saa moja asubuhi hadi saa 12 jioni.   "Watanzania na wana CCM kesho hapa uwanja wa Jamhuri tuna jambo letu tunawakaribisha wote.Kesho tunataka kuisimamisha Tanzania,Afrika na Dunia kwa kuelezea mafanikio ambayo yamepatika katika kipindi cha miaka mitano chini ya jemedari wetu Dk.John Magufuli,"amesema Polepole na kusisitiza watu watafurika uwanjani hapo kuanzia saa 12 asubuhi. Amesema kwamba baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)

KATIBU MKUU KILIMO ATEMBEELA KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA CHA MINJINGU MKOANI MANYARA

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kulia) akiongea na viongozi wa kiwanda cha mbolea cha Minjingu cha Manyara leo alipowatembelea kukagua uzalishaji.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Tosky Hans Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha mbolea cha Minjingi Bw.Tosky Hans leo alipowasili kiwandani hapo mkoani Manyara kwa ziara ya kukagua hali ya uzalishaji mbolea. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto ) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha Kahela Feeders cha Arusha Bw.Alex Kahela ( kulia) kuhakikisha anasajili bidhaa zake kwenye mamlaka za ubora ili zitambulike kwenye soko .(Picha na habari Wizara ya Kilimo) Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika chupa ya mbolea ya maji (Booster) inayozalishwa na kiwanda cha Keen Feeders cha Arusha leo alipotembelea.Akiwa kiwandani hapo ameagiza bidhaa zote hizo zisajiliwe na kupata nembo ya ubora kabla hazijaingizwa sokoni ili kuml

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI ZAKE MBAGALA ZAKHEM, DAR ES SALAAM

Image
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua rasmi kampeni zake kwenye uwanja wa Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2020. Katika uzinduzi huo Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama hicho, Tundu Lissu pamoja na mgombea mwenza wake, Salum Mwalimu walihutubia katika wafuasi wa chama hicho na wananchi waliokusanyika katika viwanja hivyo. Kampeni hizo zitaendelea hadi Oktoba 27, 2020 na uchaguzi utafanyika Oktoba 28, 2020 ili kumchagua Rais wa Jamhuri, ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Mgomeba kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu, akihutubia mkutano w akampeni wa chama hicho kwenye uzoinduai wake uliofanyika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam Agosti 28, 2020.    

OPE YAKABIDHI BAISKELI KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA JAMII VITA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO KISHAPU

Image
  Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli  Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwanima kata ya Busangwa Maneno Mahenge (kulia). Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli  Mwezeshaji wa Jamii kata ya Busangwa, Mary Solo  (kulia). Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Shirika la Organization of People Empowerment (OPE) limekabidhi baiskeli tano kwa wawezeshaji ngazi ya jamii kata ya Busangwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ili kusaidia kuifikia jamii kutoa elimu ya masuala ya ulinzi wa mtoto,mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Akizungumza leo Ijumaa Agosti 28,2020 Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya amesema shirika hilo wawezeshaji ngazi ya jamii watatumia baiskeli hizo kuifikia jamii katika kutoa elimu ya masuala ya ulinzi wa mtoto,uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. “Shirika la OPE tunatekeleza mradi wa Kutokomeza mimba na ndoa za utotoni

JKCI YAFANYA UPASUAJI WA AXILLOBIFEMORAL BYPASS GRAFT SURGERY KWA MARA YA KWANZA

Image
NA MWANDISHI   MAALUM – DAR ES SALAAM MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kutoka kwenye mshipa wa damu wa kifuani na kupeleka kwenye mishipa ya damu ya miguuni (Axillobifemoral Bypass Graft  Surgery). Upasuaji huo ni wa kwanza kufanyika hapa nchini ambapo mgonjwa alikuwa na tatizo la kupata maumivu makali maeneo ya miguuni, mapaja na sehemu ya kukalia kwa muda wa miezi nane baada ya uchunguzi ikagundulika mshipa wake mkubwa wa damu (Abdominal  Aorta)  umeziba kabisa na hivyo kushindwa kupeleka damu kwenye miguu  (Aortoilliac Occlusion Disease) damu ilikuwa inapelekwa  kupitia mishipa midogo (Collaterals). Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jijini Dar es Salaam daktari bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph alisema walimpokea mgonjwa huyo wiki iliyopita kutoka Hospitali

TANZANIA YAPOKEA SH. BILIONI 34 KUTOKA KUWAIT KUTEKELEZA MRADI WA UMWAGILIAJI LUICHE KIGOMA

Image
NA PETER HAULE NA JOSEPHINE MAJURA, WFM, DODOMA SERIKALI ya Tanzania imepokea mkopo wa masharti nafuu wa Dinar milioni 4.5 sawa na Shilingi bilioni 33.9 kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED), kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la Mto Luiche mkoani Kigoma. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja. Bw. Mwaipaja alisema kuwa Mkataba huo umesainiwa nchini Kuwait kati ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Bi. Aisha Amour, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa KFED, Abdulwahad Ahmed Al- Bader, kwa niaba ya Serikali ya Kuwait. “Fedha hizo za mkopo zitatumika katika uhakiki wa usanifu wa kina wa mradi na usimamizi wa ujenzi wa bwawa la maji la mita 375 lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo milioni 70 za maji”, alisema Bw. Mwaipaja. Alisema kuwa fedha hizo pia zitatumika katika ujenzi wa miundombinu kama mifereji ya maji, kinga za mafuriko, daraja na baraba

NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI AKUNWA NA MAFUNZO KAZINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti, 2020. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, akimshukuru Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani, Neema Shosho, kwa ufadhali wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti, 2020. Naibu Katibu  Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli akisisitiza umuhimu wa ubora wa Uratibu wa shughuli za serikali wakati akifunga rasmi  mafunzo ya kujenga uwez