NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI AKUNWA NA MAFUNZO KAZINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akisisitiza
kuwa Ofisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi
hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa ufanisi na weledi.
Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya
mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti, 2020.
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, akimshukuru
Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani, Neema Shosho, kwa ufadhali wa mafunzo
ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu
waliyokasimiwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya Mafunzo
kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti,
2020.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu,
Gerald Mweli akisisitiza umuhimu wa ubora wa Uratibu wa shughuli za serikali
wakati akifunga rasmi mafunzo
ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti
2020, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Uwekezaji), Dorothy Mwaluko na kulia ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa
Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) Dickson Mwanyika,
Maafisa wa Ofisi
ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo
leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano,
yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa
njia ya mtandao (TaGLA).
Maafisa wa Ofisi
ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo
leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano,
yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa
njia ya mtandao (TaGLA).
Mchumi
Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu. Frank Mwenga, akieleza umuhimu wa
mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo wakati wa kufunga
mafunzo hayo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo
ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya
Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
Mchumi Ofisi ya
Waziri Mkuu. Elilanga Kaaya,
akieleza umuhimu wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo
wakati wa kufunga mafunzo hayo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti
2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na
kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu
Gerald Mweli, akimkabidhi cheti Afisa Habari Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu Isabela Katondo,
baada ya kuhitimu mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji na
Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti
2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na
kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu
Gerald Mweli, akimkabidhi cheti Afisa Utumishi Ofisi ya Waziri Mkuu Herman Chando, baada ya kuhitimu
mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na
Uandishi wa Taarifa, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo
hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala
ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
OFISI ya Waziri Mkuu imefanya mafunzo ya kujenga uwezo wa
kutekeleza majukumu waliyokasimiwa kwa maafisa 36 kutoka idara na vitengo vya
ofisi hiyo. Mafunzo hayo ya wiki moja yamefanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28
Agosti 2020, Jijini Dodoma, ambapo Wakala wa Serikali ya Mafunzo kwa Njia ya
Mtandao (TaGLA) waliendesha mafunzo hayo kwa ufadhili wa Shirika la Chakula Duniani.
Lengo la mafunzo hayo
lilikuwa ni kujenga uwezo kwa maafisa wake katika maeneo ya Uchambuzi wa Sera,
Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Uandishi wa taarifa. Mafunzo hayo pia
yamewezesha maafisa hao kuongeza umahiri wa utekelezaji majukumu waliyokasimiwa
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 52, ambapo jukumu la msingi la Ofisi hiyo ni
kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali katika sekta zote na Bungeni pamoja
na majukumu mengine yaliyoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 144 Aprili
2016, lililofanyiwa mabadiliko tarehe 7 Oktoba 2017.
Akiongea wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, leo tarehe
28 Agosti jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli hakusita kueleza furaha yake juu ya
utaratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendesha mafunzo kwa watumishi yanayolenga
kujenga uwezo wa kutekeleza majukumu waliyokasimiwa.
“Nimevutiwa sana na mbinu zilizotumika katika ufundishaji
wa mafunzo haya. Nimeambiwa katika kuhakikisha mnapata mbinu na umahiri kwenye
Tathmini na Ufuatiliaji wa Sera, mmepitia Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa masuala
ya Lishe. Naelewa Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo mratibu wa mpango huu na sisi
TAMISEMI tunatekeleza. Nakusudia na mimi Kufanya mafunzo kama haya kwa
watumishi wa wizara yangu” amesisitiza Mweli.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Uwekezaji), Dorothy Mwaluko amelishukuru Shirika la Chakula Duniani kwa ufadhili
wa mafunzo hayo, ambapo matokeo ya mafunzo hayo ni Ofisi hiyo
kuwa na mfumo bora wa uratibu wa shughuli za serikali kutokana na mamlaka iliyonayo kikatiba ya kuratibu
shughuli zote za Serikali pamoja na masuala mtambuka ikiwemo masuala ya lishe.
“Mafunzo haya yatakuwa
ni mwendelezo kwa maafisa wote na menejimenti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu, lengo ni kuongeza umahiri kwa uchambuzi bora wa sera, ufuatiliaji na
tathmini ya sera pamoja na kuwa na mfumo bora wa mawasiliano ya
utekelezaji wa majukumu kwa idara zote ndani ya Ofisi, pia na mfumo bora wa
uratibu wa shughuli za serikali” amesisitiza Mwaluko.
Awali akiongea kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika amefafanua kuwa mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa utaratibu wa mijadala washiriki walipata fursa ya kufahamu mbinu za kimkakati za uchambuzi wa Sera na kanuni za uratibu wa Sera, njia za kufanya ufutiliaji na tathmini, vigezo vya kuzingatia katika kufanya tathmini na ufuatiliaji pamoja na namna ya kuandika taarifa na muundo wa taarifa.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
kwenye mafunzo hayo, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, Frank Mwega na
Elilanga Kaaya wamebainisha kuwa mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa
washiriki katika kuwajengea uwezo. Aidha, wameshauri uendelevu wa mafunzo ya
namna hiyo yenye kuwajengea uwezo watumishi kwenye maeneo ya utendaji.
Comments
Post a Comment