KATIBU MKUU KILIMO ATEMBEELA KIWANDA CHA KUZALISHA MBOLEA CHA MINJINGU MKOANI MANYARA
Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kulia) akiongea na viongozi wa kiwanda cha mbolea
cha Minjingu cha Manyara leo alipowatembelea kukagua uzalishaji.Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Tosky Hans
Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha
mbolea cha Minjingi Bw.Tosky Hans leo alipowasili kiwandani hapo mkoani Manyara
kwa ziara ya kukagua hali ya uzalishaji mbolea.
Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto ) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa
kiwanda cha Kahela Feeders cha Arusha Bw.Alex Kahela ( kulia) kuhakikisha
anasajili bidhaa zake kwenye mamlaka za ubora ili zitambulike kwenye soko .(Picha
na habari Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika chupa ya mbolea ya maji (Booster) inayozalishwa na kiwanda cha Keen Feeders cha Arusha leo alipotembelea.Akiwa kiwandani hapo ameagiza bidhaa zote hizo zisajiliwe na kupata nembo ya ubora kabla hazijaingizwa sokoni ili kumlinda mkulima.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Dkt. Stephano Ngailo (aliyesimama) akitoa
maelezo kuhusu viwanda vya mbolea za maji leo katika kiwanda cha Keen Feeders
Arusha.Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya alitembelea kiwanda
hicho (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Keen Feeders
Bw.Alfred Massawe.Kiwanda hicho huzalisha lita 600,000 za mbolea maji (boosters)
kwa mwaka.
Comments
Post a Comment