Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI AGOSTI 29, 2020

Image
 

RAIS SAMIA KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI MJINI UNGUJA, ZANZIBAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye tamasha la Kizinkazi mjini Unguja leo Agosti 28, 2021 ambapo pia  alizindua miradi mbalimbali ya maendeleo.  

RAIS HAJAWAKATAZA KUPANGA MIJI: UMMY MWALIMU AWAAMBIA MA RC

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu  amewaeleza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuwa Mhe. Rais SamiaSuluhu Hassan hajakataza kupanga Miji ila kinachotakiwa unapohamisha Wafanyabiashara lazima ujiulize he  unakowapeleka kunawafaa?Je wataendelea kupata wateja kama ilivyokuwa sehemu ulipowahamisha? Yakitimia haya inatosha kuchukua hatua ya Kupanga Miji.  

WAZIRI NDAKI AZINDUA MFUMO WA UKAGUZI WA MIFUGO, AONYA WATEKELEZAJI KUTOGEUKA KUWA POLISI

Image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), (wa pili kutoka kulia) akizindua rasmi mfumo wa ukaguzi wa mifugo na mazao yake katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma na kuwataka watekelezaji wa mfumo huo kutogeuka kuwa Jeshi la Polisi au mahakama.  (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi). Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (Mb), akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo wa ukaguzi wa mifugo na mazao yake iliyofanyika jijini Dodoma na kubainisha kuwa mfumo utaboresha na kuongeza thamani mazao ya mifugo nchini.  (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi). Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia mifugo Bw. Amosy Zephania akifafanua juu ya mfumo wa ukaguzi wa mifugo na mazao yake ambao umewezesha kufanyika mapitio ya sheria tatu za Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama ya mwaka 2010, Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003 na Sheria ya Veterinari ya mwaka 2003 na kanuni 12. Hafla fu

NIC YATOA VESTI ANGAVU NA VIBAO VYA 'STOP' , 'GO' KUZUIA AJALI KWA WANAFUNZI SHULE ZILIZOPO KANDO YA BARABARA

Image
  Meneja wa  Shirika la Bima la Taifa ( NIC)  Mkoa wa Shinyanga Hamis Iddy Mohamed (kushoto) akikabidhi sehemu ya  Vibao vinavyoonesha Ishara ya ‘STOP’ na ‘GO’  kwa  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Joseph Paul (kulia)  kwa ajili ya  wanafunzi wa shule 50 za Mkoa wa Shinyanga zilizopo kando ya barabara wavuke salama pindi wanapokwenda na wanapotoka shuleni.

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI AGOSTI 28, 2021

Image
 

WATAALAMU WA SEKTA YA AFYA KATIKA MASUALA YA UHAKIKI WA UBORA, USALAMA WA AFYA NA KUJIANDAA NA MAGONJWA YA MILIPUKO WAKUTANA DAR ES SALAAM

Image
  Kikao kazi cha wadau wa Sekta ya Afya kimeanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Seascape, kikikuhusisha wataalamu katika masuala ya Uhakiki Ubora, Usalama wa Afya na Kujiandaa na Magonjwa ya Mlipuko. Kikao hicho kimelenga kujadili masuala na changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na kupendekeza hatua za kuchukua ili kuongeza tija na ubora katika utoaji wa Huduma za Afya nchini kupitia wadau ikiwemo Sekta Binafsi. Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Dkt. Eliudi S. Eliakimu, Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kwa niaba ya Wizara ya Afya, amesema mkutano huo ni muhimu kwa wadau wa afya kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu ubora na usalama wa huduma za Afya, na kwamba kupitia mkutano huo Wizara imekuwa inapokea mrejesho na kupokea mapendekezo mbalimbali ya wadau kuhusu kuboresha utoaji wa huduma za Afya, pamoja na kukubaliana hatua za kuchukua ili kuongeza ubora wa huduma na udhibiti wa magonjwa. “ Pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwem

SERIKALI YATENGA BILIONI 41.87 MIRADI YA UMEME RUKWA

Image
 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga takribani shilingi bilioni 41.87 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini mkoani Rukwa. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo Agosti 26, 2021 alipokuwa akizindua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa  pili katika kijiji cha Lowe kata ya Lusaka Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa. Fedha hizo zitatekeleza miradi ya umeme kwenye vijiji  339 katika mkoa wa Rukwa.  Aidha, Dkt. Kalemani amesema kuwa, Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1.24. kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji  wa miradi ya umeme Vijijini awamu ya tatu  mzunguko wa pili hadi kufikia mwezi septemba mwaka 2022. "Tanzania imefikia asilimia 86 ya usambazaji wa umeme katika vijiji na kuifanya kuwa ya kwanza Afrika kwa kusambaza umeme vijijini" alieleza Dkt. Kalemani.