SERIKALI YATENGA BILIONI 41.87 MIRADI YA UMEME RUKWA


 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga takribani shilingi bilioni 41.87 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini mkoani Rukwa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo Agosti 26, 2021 alipokuwa akizindua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa  pili katika kijiji cha Lowe kata ya Lusaka Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Fedha hizo zitatekeleza miradi ya umeme kwenye vijiji  339 katika mkoa wa Rukwa. 
Aidha, Dkt. Kalemani amesema kuwa, Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1.24. kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji  wa miradi ya umeme Vijijini awamu ya tatu  mzunguko wa pili hadi kufikia mwezi septemba mwaka 2022.
"Tanzania imefikia asilimia 86 ya usambazaji wa umeme katika vijiji na kuifanya kuwa ya kwanza Afrika kwa kusambaza umeme vijijini" alieleza Dkt. Kalemani.





 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"