CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"
NA MWANDISHI WETU NA MASHIRIKA YA HABARI KOCHA mpya wa Simba, Pablo Franco Martin, mzaliwa wa Madrid, nchini Hispania, ndiye kocha mwenye CV iliyosheheni kuwahi kutokea katika historia ya soka hapa nchini. Pablo Franco, alizaliwa Juni 11, 1980 katika jiji la Madrid, na hadi “Anatangazwa kuja” kwa Wekundu wa Msimbazi Simba, kocha huyo ana leseni ya UEFA Pro Licence ambayo inaelezwa kuwa ndiyo leseni inayotolewa kwa muhitimu wa mafunzo ya juu kabisa ya Ufundishaji (Coaching) na Usimamizi (Managerial) wa wa soka barani Ulaya. Kocha huyo kijana ni miaka minne tu iliyopita alikuwa akifanya kazi na Kocha mwenye mafanikio makubwa Duniani kwenye mpira wa miguu akiwa kama mchezaji na kocha, Maestro Zinedine Zidane “Zizou” kwenye Klabu ya Real Madrid ya Uhispania kama kocha msaidizi. Kocha Pablo mbali na kuiongoza Real Madrid kam Kocha Msaidizi, aliwahi pia kufundisha timu za Getafe CF na Getafe B zote za Hispania, pia timu za Club Deportivo Santa Eugenia, Club Deportivo Illescas,
Comments
Post a Comment