WATAALAMU WA SEKTA YA AFYA KATIKA MASUALA YA UHAKIKI WA UBORA, USALAMA WA AFYA NA KUJIANDAA NA MAGONJWA YA MILIPUKO WAKUTANA DAR ES SALAAM

 

Kikao kazi cha wadau wa Sekta ya Afya kimeanza leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Seascape, kikikuhusisha wataalamu katika masuala ya Uhakiki Ubora, Usalama wa Afya na Kujiandaa na Magonjwa ya Mlipuko. Kikao hicho kimelenga kujadili masuala na changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na kupendekeza hatua za kuchukua ili kuongeza tija na ubora katika utoaji wa Huduma za Afya nchini kupitia wadau ikiwemo Sekta Binafsi.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Dkt. Eliudi S. Eliakimu, Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kwa niaba ya Wizara ya Afya, amesema mkutano huo ni muhimu kwa wadau wa afya kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu ubora na usalama wa huduma za Afya, na kwamba kupitia mkutano huo Wizara imekuwa inapokea mrejesho na kupokea mapendekezo mbalimbali ya wadau kuhusu kuboresha utoaji wa huduma za Afya, pamoja na kukubaliana hatua za kuchukua ili kuongeza ubora wa huduma na udhibiti wa magonjwa.

“ Pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa UVIKO – 19 uliosababisha wadau kutokutana kwa muda mrefu, tunashukuru Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia mradi wa CDC - PEPFAR waliofadhili mkutano huu muhimu kwa wadau, ambao baadhi ya wadau wengine wameweza kushiriki kwa njia ya mtandao”. Alisema

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Henry A. Mollel Mratibu na msimamizi wa mradi wa CDC – PEPFAR amesema “Chuo Kikuu Mzumbe kitaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya afya kuboresha mifumo ya afya nchini, kupitia wataalamu wake waliopo kwenye Kituo Bora cha Ufuatiliaji na Tathmini ya Mifumo na Miradi ya Afya, chini ya Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti, pamoja na kuendelea kufadhili mikutano ya wadau wa Afya, chini ya mradi wa CDC -  PEPFAR.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mkutano huo wameshukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwezesha kikao hicho kufanyika, kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo kwa sasa kwenye Sekta ya Afya, ambayo yanahitaji majadiliano na makubaliano ya pamoja, ambayo yatatoa mjumuisho na fursa ya kurekebisha masuala mengi ya kisekta, pamoja na kuongeza ubora katika udhibiti, uhakiki na ukaguzi wa mifumo mbalimbali ya utoaji huduma za Afya nchini.

Zaidi ya washiriki thelathini wameshiriki kitika kikao hicho na wengine 20 wameshiriki kwa njia ya mtandao, kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI, wawakilishi kutoka  shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa (CDC), Taasisi ya Taifa ya Utafiti na Tiba (NIMR), USAID, AMREF, UNICEF, GTZ, CSSC, Engender, MDH, AGPAHI, Pharmaccess, EGPAF, Chuo Kikuu Mzumbe na wengineo.  Kikao kazi hiki kimefanyika kwa mara ya kwanza tangu kilipofanyika kwa mara ya mwisho miaka miwili iliyopita, kutokana na changamoto za rasilimali na  ugonjwa wa UVIKO -  19.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu akizumgumza na wadau mbalimbali Sekta ya Afya wakati  akifungua kikao kazi cha wadau wa Sekta ya hiyo leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  Hoteli ya Seascape.Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa CDC – PEPFAR kutoka  Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Henry A. Mollel akizumgumza na wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya juu  kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya afya ili kuboresha mifumo ya afya nchini wakati wa kufungua kikao kazi cha wadau wa Sekta ya hiyo  leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  Hoteli ya Seascape.Mratibu na Msimamizi wa Mradi wa CDC – PEPFAR kutoka  Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Henry A. Mollel (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu wakati wa kufungua kikao kazi cha wadau wa Sekta ya Afya  leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  Hoteli ya Seascape.


Baadhi ya wadau mbalimbali  wa Sekta ya Afya  wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu (hayupo pichani)  wakati akifungua  kikao kazi cha wadau wa Sekta ya hiyo leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  Hoteli ya Seascape.
Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya,Dkt. Eliudi S. Eliakimu (katikati) akiwa katika picha ya pamaoja na wadau wa Sekta ya Afya leo Agosti 26, 2021. jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa  Hoteli ya Seascape. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"