Posts

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA IDARA YA AFRIKA- IMF IKULU, DODOMA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan   akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF-) Abebe Aemro Selassie Ikulu Jijini Dodoma leo tarehe 29 Juni, 2021. Mkurugenzi wa Idara ya Afrika (IMF) Abebe Aemro Selassie akizungumza na Wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika Ikulu Jijini Dodoma leo tarehe 29 Juni, 2021. ( PICHA NA IKULU).

TANZIA: INJINIA MFUGALE AFARIKI DUNIA

Image
 

MAONESHO YA 45 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR E SALAAM: PSSSF YAJA KIVINGINE, WANACHAMA NA WANANCHI WAKARIBISHWA KUPATA TAARIFA ZA KUMILIKI NYUMBA

Image
 NA MWANDISHI WETU. MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewaalika wanachama wake na wananchi kwa ujumla kutembeela banda la Mfuko huo ili kupata taarifa za huduma mbalimbali zikiwemo zile la kumiliki nyumba kwa gharama nafuu. Akizungumza kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Juni 29, 2021 Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Bw. James Mlowe alisema, Mfuko umedhamiria kwa dhati kuhakikisha unawawezesha wanachama wake na wananchi kwa ujumla kumiliki nyumba na viwanja sehemu mbalimbali nchini kwa kulipa kidogokidogo. “Tumeingia makubaliano na benki ya Azania ambayo itawawezesha wanachama na wananchi kukopa mikopo ya makazi (Mortgage loan) kwa masharti nafuu ili kununua nyumba na viwanja vinavyomilikiwa na PSSSF  kupitia uwekezaji iliyoweka sehemu mbalimbali nchini kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Shinyanga,

TUNDU LISSU AFURAHISHWA NA UONGOZI WA RAIS SAMIA NDANI YA SIKU 100

Image
  Rais Samia Suluhu Hassan WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitimiza siku 100 kama Rais wan chi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu amefurahishwa na mambo kadhaa ambayo Rais ameyafanya. Akihojiwa kwenye kipindi cha Amka na BBC leo asubuhi Juni 29, 2021, Mhe. Lissu alisema mabadiliko makubwa ya kauli na vile vile ile healing ya watu kuna faraja kubwa, taifa limepumua kwa sababu Mamam Samia Suluhu Hassan yuko tofauti sana kwa kauli, anazungumza taratibu hatishii watu, vyombo vya habari vimeanza kuandika vitu ambavyo hawakuwa wakiviandika hapo kabla, alisema. “Kuna baadhi ya vitu ambavyo amevifanya ambavyo vimeongeza faraja mfano msimamo wake kuhusu ungonjwa wa Covid19 ambao umeua watu wengi duniani nchi ilikuwaimefika mahali   imekwama, mama amebadilisha hiyo hali tunaelekea kwenye ushirikiano na majirani zetu, ushirikiano na Jumuaiya ya Kimataifa na Shirika la Afya Duniani katika kukabiliana na hu

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE JUNI 29, 2021

Image
 

TGNP YAPONGEZA KASI YA RAIS SAMIA SIKU 100

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi  Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amepongeza mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akisema inazingatia masuala ya usawa wa kijinsia hali itakayosababisha maendeleo yaende kwa haraka.

WAZIRI MKENDA AONESHA WAZI KUTORIDHISHWA NA MWENENDO WA KNCU// ASEMA SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA YA USHIRIKA YA MWAKA 2013

Image
  Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU)  tarehe 28 Juni 2021,  uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.  (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU)  tarehe 28 Juni 2021,  uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, Ndg Geoffrey Kirenga   akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU)  tarehe 28 Juni 2021,  uliofanyika katika Ma

MAKONSELI WAKUU WA MSUMBIJI NA OMAN WAWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

Image
Na mwandishi wetu. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula apokea nakala ya hati za utambulisho za Makonseli Wakuu wawili kutoka Msumbiji na Oman wenye makazi Zanzibar. Makonseli hao ni Mhe. Agustinho Abacar Trinta Konseli Mkuu wa Msumbiji pamoja na Mhe. Said Salim Al Sinawi Konseli Mkuu wa Oman Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamedajiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya nchi zao na Tanzania. Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasilisha nakala ya hati za utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Oman mwenye makazi Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi. Uwa

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAKATI AKITIMIZA SIKU 100 TANGU AINGIE MADARAKANI

Image
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 28, 2021 amekutana na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati akitimiza siku 100 tangu aingie madarakani, Mhe. Rais alianza mkutano wake kwa kupokea maoni na maswali kutoka kwa Wahariri wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile. Baada ya kupokea maoni na maswali hayo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alitoa hotuba fupi na kumkaribisha Mhe. Rais ambaye alijibu maswali hayo na kuelezea dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza kuwa itashirikiana kwa karibu na vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yake na kwa kuonyesha hilo, Rais ameagiza magazeti ambayo yalimaliza adhabu yake ya kufungiwa yatakapokamilisha usajili yaachiwe yaendelee na jukumu lake la kuhabarisha. Rais pia ametoa changamoto kwa vyombo vya habari kuchangamkia fursa za matangazo kutoka Taasisi za Umma na Binafsi na kuwaondoa shaka kuwa haku