TUNDU LISSU AFURAHISHWA NA UONGOZI WA RAIS SAMIA NDANI YA SIKU 100
WAKATI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitimiza
siku 100 kama Rais wan chi, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu amefurahishwa na mambo kadhaa ambayo Rais
ameyafanya.
Akihojiwa
kwenye kipindi cha Amka na BBC leo asubuhi Juni 29, 2021, Mhe. Lissu alisema
mabadiliko makubwa ya kauli na vile vile ile healing ya watu kuna faraja kubwa, taifa limepumua kwa sababu Mamam
Samia Suluhu Hassan yuko tofauti sana kwa kauli, anazungumza taratibu hatishii
watu, vyombo vya habari vimeanza kuandika vitu ambavyo hawakuwa wakiviandika
hapo kabla, alisema.
“Kuna
baadhi ya vitu ambavyo amevifanya ambavyo vimeongeza faraja mfano msimamo wake kuhusu
ungonjwa wa Covid19 ambao umeua watu wengi duniani nchi ilikuwaimefika mahali imekwama, mama amebadilisha hiyo hali
tunaelekea kwenye ushirikiano na majirani zetu, ushirikiano na Jumuaiya ya
Kimataifa na Shirika la Afya Duniani katika kukabiliana na huu ugonjwa
unaoikabili dunia nzima hilo ni jambo jema sana.”
“Vilevile
mama alisema yeye hataki kuona watu wakikamatwa bila sababu na kufunguliwa kesi
za kubambikia na pia ameachilia watu waliokuwa wameshikiliwa kwa muda mrefu wakiwemo
masheikh wa Uamsho Zanzibar.” Alisema.
Hata
hivyo Mhe. Lissu amehimiza uwepo wa Katiba mpya “Tulitakiwa tuwe na Katiba mpya baada ya tume ya Rais iliyoleta nchi
kwenye mfumo wa vyama vingi , tume ya Jaji Nyalali iliyopendekeza tuwe na
Katiba mpya mwaka 1991 hili suala la Katiba mpya lilipaswa liwe siyo swala la
kujadiliwa leo.” Alisema.
Akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu Juni 28,
2021 Rais Samia aliwaahidi watanzania kuwa Katiba mpya ni suala muhimu lakini
kwa sasa ameomba apewe muda kulishughulikia.
Rais
Samia aliapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano marehemu Dkt.
John Pomba Magufuli Machi 17, 2021.
Comments
Post a Comment