RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAKATI AKITIMIZA SIKU 100 TANGU AINGIE MADARAKANI
Baada ya kupokea maoni na maswali hayo, Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alitoa hotuba
fupi na kumkaribisha Mhe. Rais ambaye alijibu maswali hayo na kuelezea dhamira
ya Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza kuwa itashirikiana kwa karibu na
vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yake na kwa kuonyesha hilo, Rais
ameagiza magazeti ambayo yalimaliza adhabu yake ya kufungiwa yatakapokamilisha
usajili yaachiwe yaendelee na jukumu lake la kuhabarisha.
Rais pia ametoa changamoto kwa vyombo vya
habari kuchangamkia fursa za matangazo kutoka Taasisi za Umma na Binafsi na
kuwaondoa shaka kuwa hakuna mahala popote ambapo serikali ilitoa maelekezo
maalum ya kuvinyima vyombo vya habari vya binafsi matangazo ya biashara kutoka
serikalini.
Comments
Post a Comment