DC SAME AHIMIZA UBUNIFU KATIKA UKUSANYAJI MAPATO WILAYANI HUMO
NA ASHRACK MIRAJI, SAME Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Mhe. Kasilda Mgeni, ameagiza Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kutumia ubunifu, weledi pamoja na busara katika kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waadilifu. Mkuu huyo wa Wilaya amebainisha hayo katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi cha Wilaya na kusisitiza kuwa mfanyabiashara yeyote atakaye bainika kuendelea kukiuka kulipa kodi taarifa iwasilishwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Amesema suala la ulipaji kodi ni wajibu wa kila mwananchi kisheria ili kusaidia Serikali kupanga shughuli za kuwaletea wananchi wake maendeleo. “TRA fanyeni operesheni za mara kwa mara kwa wafanyabiashara wote ambao wapo ndani ya Wilaya ya Same na wanaostahili kutumia mashine za Kielektroniki (EFD) basi wanakuwa nazo na kwa wale ambao watakuwa wakaidi baada ya kuwafuatilia na kuwapa elimu basi sheria iweze kuchukua mkondo wake juu yao kwa