WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE VYA KUONDOA CHANGAMOTO ZA ARDHI
Na Munir Shemweta, WANMM Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wizara yaje imeweka vipaumbele 12 katika mwaka ujao wa fedha 2023/2024 unaoanza Julai mosi mwaka huu lengo kubwa likiwa kuondoa changamoto za sekta ya ardhi na kutilia mkazo ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi. Kwa mujibu wa Dkt Mabula katika kipindi cha mwaka huo wa fedha wa 2023/2024, Wizara ya Ardhi imejipanga kuhakikisha mikakati yake inaenda vizuri hususan kuondoa kero na malalamiko ya wananchi kwani dhamira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha nchi inakuwa kiuchumi na watu wake wanafaidika na mali waliyokuwa nayo ambayo ni ardhi. Dkt Mabula alisema hayo jana tarehe 28 Juni 2023 ikiwa ni muda mfupi baada ya kikao cha uongozi wa wizara kwa ajili ya kuweka mikakati ya kutekeleza vipaumbele vya Wizara ya Ardhi baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti 2023/2024 ambapo kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi kabla ya viongozi kuanza kusambaa maeneo mbalimbali