MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA WAUKINI WA KIISLAMU KATIKA SALA YA EID AL ADHA HUKO UNGUJA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Alhamis Juni 29, 2023 amewaongoza Waumini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Idd al Adh-ha hapo Masjid Mushawwar,  Mskiti uliopo Muembeshauri Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja. 

Viongozi mbali mbali  wamehudhuria katika Sala hiyo akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla; Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita (6) wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabhi 

Sikukuu ya Idd al Adh-ha inakuja baada ya kukamilika kwa Ibada ya Hijja, Nguzo ya 5 ya Dini ya Kiislamu, inayofanyika huko Makka Saudi Arabia. 






Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"