RC KUNENGE APOKEA NG'OMBE 500 ,MBUZI 1,000 KWA AJILI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA

 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

Mkuu wa mkoa wa Pwani , alhaj Abubakari Kunenge, amepokea  Ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 kutoka Jumuiya ya IDDEF ya nchini Uturuki wakishirikiana na Rahma Fondation ya Tanzania kwa ajili ya sadaka ya sikukuu ya Eid Al Adha .
Akikabidhi Sadaka hiyo ,Sheh Bahadhir kutoka katika taasisi hiyo, katika machinjio ya Pangani, mjini Kibaha, alisema IDDEF , taasisi ya Rahmah ya nchini Tanzania wametoa ng'ombe na mbuzi hao kwa ajili ya  Sadaka hiyo hususan kwa wajane,yatima na wazee.
Aidha aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali msaada huo na kutoa machinjio hiyo kwa ajili ya kuchinjia wanyama hao.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa Kunenge, aliishukuru taasisi hizo kwa sadaka hiyo ya ibada ya kuchinjwa ya Eid Al  adha na kwamba sadaka hiyo itagawanywa kwa wahitaji ikiwemo, yatima,wajane na wazee.
"Nimepokea Ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 Kwa ajili ya sadaka ya ibada ya kuchinjwa ya EId Al Adha  naipongeza Jumuiya hii Rahma Foundation na IDDER na mashekh wote kutoka Uturuki kwa kuendelea kushirikiana na nchi yetu katika nyanja mbalimbali"alisema Kunenge.
Licha ya hayo Kunenge alieleza ni vema Sadaka hizo zikatolewa Kwa wahitaji ikiwemo yatima,wajane, wazee, watu wasiojiweza na waalimu wa dini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Shekh wa Mkoa wa Pwani, Salimini Buda,aliishukuru taasisi hiyo na kwamba Sadaka hiyo itawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"