VYOMBO VYA HABARI VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA SEKTA YA UCHUMI NA FEDHA-NAIBU GAVANA BoT JULIAN BANZI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID NAIBU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani, Bw. Julian Banzi amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuelimisha umma kuhusu masuala ya Uchumi na Fedha. Akizungumza kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu wakati akifungua Semina ya siku moja ya masuala ya Uchumi na Fedha, kwa wahariri wa vyombo vya habari kwenye Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam leo Februari 27, 2023, Bw. Banzi alisema, BoT ina amini kuwa wahariri na waandishi wa habari wakiwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya Fedha na Uchumi, watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufikisha ujumbe ulio sahihi na kwa lugha rahisi kwa wananchi. Alisema, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria inayoipa BoT mamlaka ya kusimamia Sekya ya Huduma Ndogoz a Fedha. Chini ya Sheria hiyo BoT ndiyo inayosajili, Kusimamia na Kudhibiti biashara ya huduma ndogo za Fedha Tanzania Bara. "Hapo nyuma kulikuwa na changamoto kidog