UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM GOBA, MTEMVU ASEMA CCM ITAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU, AMPONGEZA DIWANI ESTHER NDOHA

 

 NA MWANDISHI WETU.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi,CCM Mkoa wa Dar es salaam Abass Mtemvu amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuboresha mazingira ya huduma za elimu,afya na barabara

Mtemvu ameyasema hayo leo jumapili februari 26 alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu maalum wa CCM kata ya Goba na kuongeza kuwa kipaumbele chake katika mkoa huo ni Kuhakikisha maeneo yote ya Mkoa huo yanapata miundombinu bora ya barabara za uhakika za lami.

Ameongeza kuwa chama hicho kitahakikisha mpaka kufikia mwaka 2024 maeneo yote ya Mkoa wa Dar es salaam yanakuwa na miundombinu ya uhakika ikiwemo ya maji safi na salama ya uhakika ambayo yatachangia wakaazi wote kupata huduma hiyo muhimu ya maji.

Kuhusu makampuni ya urasimishaji na upimaji ardhi ambayo yameshindwa kufanya kazi hiyo ndani ya kata ya Goba licha ya kulipwa fedha kutoka kwa wananchi,mwenyekiti huyo amesema kuwa atakutana na Mkuu wa mkoa huo hapo kesho na kuyataka makampuni hayo ama yakamilishe kazi ya urasimishaji na upimaji ardhi au kurudisha fedha za wananchi.

Aidha kuhusu suala la mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri inayotolewa kwa Wanawake,Vijana na wenye ulemavu,Bw Mtemvu amewataka wote waliopata mikopo hiyo hasa vijana kuirejesha mikopo ili wengine wapatiwe kwani baadhi yao wamekuwa hawairejeshi mikopo hiyo jambo linalokwamisha wengine kuipata.

"Nimeagiza pia wenyeviti wa mitaa wapitie majina ya akina mama na vijana na waangalie kama waliopata mikopo ni wakazi wa kata au mitaa ile na hizi pesa wengine wanafikiri ni zawadi Lah siyo za zawadi bali ni pesa zinazoingia kwenye mzunguko hivyo zirejeshwe na wenyeviti simamieni hilo la mikopo ili wanaopata pia wazirejeshe"alisema Mtemvu.

Hata hivyo Mtemvu amempongeza diwani wa kata ya Goba kwa uwasilishaji mzuri wa ripoti ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho ndani ya kata yake ili wananchi wafahamu kinachoendelea

Awali diwani wa kata ya Goba Bi Esther Ndoha akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya Kata hiyo mbele ya wajumbe hao amesema kuwa shule mpya ya sekondari ya kidato Cha 5 na 6 inayojengwa katika kata hiyo inategemewa Kuanza kuchukua wanafunzi mwaka huu ili kupunguza adha ya wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.

Diwani huyo amesema kuwa mpaka sasa shule hiyo mpya ya kidato Cha 5 na 6 yameshajengwa madarasa matatu, mabweni mawili ya wavulana na wasichana pamoja na jiko na wanaenda Ujenzi wa bwalo la Chakula ili kuifanya shule hiyo ianze kupokea wanafunzi wa kidato Cha 5 mwaka huu.

Mbali na shule hiyo pia diwani huyo aliongeza kuwa tayari pia shule mbili mpya za msingi zimeshajengwa ndani ya kata ya Goba ndani ya kipindi Cha miaka miwili ambazo ni shule ya msingi Kinzudi ambayo itafunguliwa hivi karibuni baada ya matundu ya vyoo kukamilika pamoja na shule ya msingi Matosa ambayo tayari ilishaanza kutoa huduma na sasa Ina darasa la 3 na kuifanya kata hiyo kuwa na shule 8 za msingi na 5 za sekondari.

"ndugu wajumbe ili kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu serikali imefanikiwa kujenga madarasa 47 Kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri sambamba na ruzuku za serikali Kuu katika shule za Goba ili kuziwezesha kupokea wanafunzi wote, hivyo nitoe wito Kwa wajumbe wa mashina kuhakikisha wanawahimiza wazazi kuwapeleka watoto shule sababu serikali imebiresha mazingira ya kusomea" alisisitiza diwani huyo.

Kuhusu suala la Afya ndani ya kata hiyo diwani Esther Ndoha alisema kuwa katika kuboresha mazingira ya afya ambapo imepokea fedha kiasi Cha shilingi milioni 500 Kwa ajili ya Ujenzi wa kituo Cha Afya Goba ambao umefikia katika hatua za umaliziaji ambayo itasaidia kupunguza adha ya wakaazi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani kufuata huduma za Afya katika hospitali za Sinza na Mwananyamala kwani sasa watazipata katika kituo hicho kikubwa Cha Afya.

Aidha aliongeza kuwa Chama hicho kata ya Goba kinaishukuru serikali kwa kuwapeleke mradi mkubwa wa maji ambao umejengwa Kwa fedha za benki ya dunia kwa thamani ya Bilioni 5 ambao umekamilika Kwa asilimia 96% na shughuli ya ulazaji wa mabomba ya maji mitaani inaendelea,pamoja na kupima pressure na kusafisha mabomba ambayo tayari yamekwishalazwa,huku akiongeza kuwa miongoni mwa kero zinazoukumba mradi huo ni pamoja na baadhi ya wananchi kukataa mabomba kupita kwenye maeneo Yao.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"