VYOMBO VYA HABARI VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA SEKTA YA UCHUMI NA FEDHA-NAIBU GAVANA BoT JULIAN BANZI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
NAIBU
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), anayeshughulikia Utawala na Udhibiti wa Ndani, Bw. Julian Banzi amesema vyombo vya
habari vina mchango mkubwa katika kuelimisha umma kuhusu masuala ya Uchumi na
Fedha.
Akizungumza
kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu wakati akifungua Semina ya siku moja ya masuala ya Uchumi na Fedha, kwa wahariri
wa vyombo vya habari kwenye Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam leo
Februari 27, 2023, Bw. Banzi alisema, BoT ina amini
kuwa wahariri na waandishi wa habari wakiwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala
ya Fedha na Uchumi, watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufikisha ujumbe ulio
sahihi na kwa lugha rahisi kwa wananchi.
Alisema, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria inayoipa BoT mamlaka ya kusimamia Sekya ya Huduma Ndogoz a Fedha.
Chini ya Sheria hiyo BoT ndiyo inayosajili, Kusimamia na Kudhibiti biashara ya huduma ndogo za Fedha Tanzania Bara.
"Hapo nyuma kulikuwa na changamoto kidogo kwa Taasisi za huduma ndogo za fedha kama vile zinazotoa mikopo midogo midogo, vikoba hivyo Bunge lilitunga sheria ili kuondoa changamoto hizo.. Ni vizuri mkapata nafasi ya kuelezwa kuhusu sekta hiyo ndogo ya fedha na changamoto zilizokuwepo ambazo zilikuwa zinawaumiza wakopaji.” Alifafanua.
Alisema
BoT inashirikiana na vyombo vya habari kwa nia ya kufikisha ujumbe kwa wananchi
ili waweze kuelewa fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye sekta ya fedha na
hivyo kufaidika nazo.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Bakari Machumu aliishukuru BoT kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wahariri kwani yatasaidia sana katika kuongeza uelewa kuhusu masuala ya Uchumi na Fedha. Kuu.
NAIBU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Julian Banzi (kushoto), akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kwenye semina ya siku moja ya masuala ya Uchumi na Fedha iliyofanyika kwenye ukumbi wa Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam Februari 27, 2023. Kulia ni Meneja Msaidizi wa Uhusiano na Itifaki BoT, Bi. Noves Moses.NAIBU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Julian Banzi
Comments
Post a Comment