Posts

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI SAFARI YA TRENI YA ARUSHA-DAR ES SALAAM JIJINI ARUSHA LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Arusha mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa wa TRC Masanja Kadogosa mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Arusha mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza

AGIZO LA RC KUNENGE JUU YA UTOAJI WA KONTENA ZILIZOKUWA ZIMEKWAMA BANDARINI LATEKELEZWA

Image
Kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge  kuitakataasisi ya TICTS kuhakikisha kontena Sita zenye Vifaa vya Ujenzi wa Stand mpya ya Mbezi Louis zilizokuwa zimekwama Bandarin kutoka ndani ya masaa mawili, hatimae Taasisi hiyo imetekeleza mara moja agizo hilo. Mapema leo RC Kunenge amefika Stand mpya ya Mbezi Louis kujihakikishia Kama kontena hizo zimefika ambapo amethibitisha kujionea kontena zote sita zimefika na kufanya idadi kontena zilizotoka kufikia 14. Aidha RC Kunenge amebainisha kuwa kontena zilizofika ndani yake Kuna Vifaa mbalimbali ikiwemo Vioo, Fremu za madirisha, Mabati na kueleza kuwa Vifaa hivyo vimeanza kutumika Mara tu vilipofika. Hata hivyo RC Kunenge ameendelea kumtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na Mchana ili Stendi hiyo ikamilike kabla ya November 30 Kama alivyoagiza Rais Dkt. John Magufuli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi. Itakumbukwa siku ya Jana October 23 RC Kunenge alifanya ziara ya kustukiza kwenye Bandari ya Dar es salaam kuf

WATU 10 WAFA KATIKA AJALI YA BASI HUKO MKOANI KAGERA

Image
Watu 10 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa na kupelekwa hospitali teule ya Nyamiaga wilayani Ngara, Mkoani Kagera baada ya gari la abiria mali ya kampuni ya Emirates kuanguka likitokea Ngara kwenda Bukoba mapema leo Oktoba 24, 2020. Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, David Mapunda amethibitisha kupokea miili na majeruhi hao.  

WATAALAMU WA AFYA NA MAZINGIRA WATAKIWA KUJISAJILI NA KUHUISHA LESENI ZAO

Image
Na WAJMW-Dodoma Wataalamu wa Afya na mazingira nchini wametakiwa kujitokeza kujisajili na kuhuisha leseni zao ili waweze kutambulika na kupata nafasi ya kufanya kazi kwa weledi na bila usumbufu. Hayo yamesemwa na kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Eliud Eliakim wakati alipomuwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali katika ufunguzi wa kikao cha Baraza la Mazingira la awamu ya nne kilichofanyika leo katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.  Dkt. Eliud amesema Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanikiwa kuhuisha mwongozo wa maadili na nidhamu kwa watumishi wa umma ambapo kila Baraza limetakiwa kufuata mwongozo huo ili lisimamie maadili na nidhamu ya taaluma husika. Baraza la Afya ya Mazingira limetakiwa kuhakikisha wataalam wote wa Afya ya Mazingira wakiwemo maafisa afya nchini wanajitokeza kujisajili na kuhuisha leseni zao ili waweze kusimamia vyema mazingira kwa kutoa miongozo na kufanya usafi ili kuweza kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kujitokeza. Aidha, Kaimu Mganga Mkuu wa

RC KUNENGE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI, ATOA MASAA MAWILI KONTENA ZILIZOZUILIWA KUANZA KUTOKA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es salaam kufuatilia kinachokwamisha kutoka kwa kontena zenye Vifaa vya ujenzi wa Stendi ya kisasa Mbezi Louis ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alietaka ujenzi wa Stendi hiyo kukamilika kabla ya Novemba 30 mwaka huu. Katika ziara hiyo RC Kunenge amebaini udhaifu wa kiutendaji wa wakala kutoka kampuni ya Amazon General supply service na ushirikiano usiojitosheleza miongoni mwa Taasisi za umma zinazohusika kwenye mchakato mzima wa utoaji wa Mizigo bandarini. Kutokana na hali hiyo RC Kunenge ametoa masaa mawili kwa Taasisi ya TICTS kuhakikisha kontena zilizokwama zinatoka na kuwaagiza TRA kuichunguza upya kampuni ya Amazon Kama inakidhi sifa na uwezo wa kufanya kazi ya uwakala.  Aidha RC Kunenge amezielekeza taasisi za umma kuwa na ushirikiano Katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali inayolenga kutatua kero za wananchi pamoja na wateja wengine wanaotum

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI OKTOBA 24, 2020

Image
 

ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI KURAHISISHA BIASHARA MTANDAO

Image
Na Faraja Mpina WUUM, Dodoma Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) na taasisi zilizo chini ya sekta hiyo zipo katika utekelezaji wa mpango mkakati shirikishi wa kukamilisha mpango wa  anwani za makazi na postikodi unaotarajiwa kufikia halmashauri zote nchini ifikapo mwaka 2022 ili kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kidijitali. Akizungumza katika ziara ya kukagua uwekeaji wa namba za nyumba katika kata  Tatu za Chamwino Ikulu, Ipagala na Hazina, jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa ukamilishaji wa mpango huo utarahisisha shughuli za biashara mtandao na huduma za posta mlangoni. “Wizara ipo kwenye utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha kila nyumba inakuwa na anwani ya makazi inayojumuisha jina la barabara, mtaa na namba ya nyumba, ili wananchi waweze kufikiwa katika maeneo wanayoishi kwa urahisi na  kukuza biashara mtandao na posta mlangoni kuelekea uchumi wa kidijitali”,  alizungumza Dkt. Chaula. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Id