Posts

JPM AHUTUBIA WANANACHI WA MBALIZI, AOMBEWA NA MASISTER WA KANISA KATOLIKI MBEYA

Image
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Mbalizi mkoani Mbeya wakati akielekea Tundumba kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa CCM leo tarehe 01 Oktoba 2020.  Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Mbalizi mkoani Mbeya wakati akielekea Tundumba kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa CCM leo tarehe 01 Oktoba 2020.  Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Mbalizi mkoani Mbeya wakati akielekea Tundumba kwa ajili ya Mikutano ya Kampeni za Urais kwa upande wa CCM leo tarehe 01 Oktoba 2020.   Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Sala ya heri katika Majukumu yake na Masista wa Kanisa Katoliki jijini Mbeya jana mara baada ya kuwahutubia Maelfu ya Wananchi wa mkoa wa Mbeya 

ASILIMIA 70 YA WAGONJWA WANAOFIKA JKCI WANASUMBULIWA NA SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA).

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya jinsi gani unaweza kuepuka kupata magonjwa ya moyo kwa wananchi waliofika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo wilya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma  za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa. Ivan Edmund kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Philips Pharmaceuticals Tanzania Ltd. akitoa dawa kwa mwananchi aliyekutwa na tatizo la  moyo  mara baada ya kupata matibabu wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale waliokutwa na matatizo ya

TARURA YABORESHA MIUNDOMBINU WILAYANI KYERWA

Image
Muonekano wa Barabara ya Omukigando–Omukalinzi yenye urefu wa Km 6.5 ikiwa imekamilika na kuanza kutumika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera. Muonekano wa Barabara ya Omukigando–Omukalinzi kabla ya kujengwa na TARURA iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera ambapo wananchi walikuwa wanazunguka umbali mrefu kufika maeneo mbalimbali ikiwemo Nyakatuntu, Nkwenda na Omukalinzi.   Na Geofrey A. Kazaula Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera umeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara na vivuko katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Mratibu wa TARURA Mkoa wa Kagera Mhandisi Avith Theodory alisema kuwa ujenzi wa Barabara ya Omukigando – Omukalinzi yenye urefu wa Km 6.5 imesaidia kutatua kero ya muda mrefu iliyokuwa inawakabili wananchi wa Kyerwa ambao walikuwa wanatumia mtumbwi kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.  “Tunamshukuru Mtendaji Mkuu wa TARURA kwa kuto

TARI: WAKULIMA ZINGATIENI MATUMIZI YA MBEGU BORA ZA KOROSHO

Image
  Mratibu wa zao la Korosho nchini kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele, Dkt. Geradina Mzena akiwaeleza Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri mbalimbali za jiji la Dodoma jana namna bora ya kuzalisha kwa tija zao hilo. Maafisa Ugani na Wakulima wakifuatilia mafunzo hayo. Dkt. Mzena (aliyekaa wa kwanza kushoto) akiangalia korosho karanga na bibo lenye ubora lililovunwa kwa mara ya kwanza juzi na mkulima kutoka Bahi Salum Mjungu (aliyevaa miwani). Kushoto aliyesimama ni Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Bahi, Abia Silungwe. Mtafiti Mwandamizi kutoka Tari Naliendele, Dkt. Wilson Nene akiwafundisha maafisa ugani na washiriki namna ya kutambua aina za magonjwa na wadudu waharibifu wa zao la korosho kupitia moja ya mkorosho ambao umeathiriwa vibaya na ugonjwa wa ‘Die Back’. Mkulima wa Korosho kutoka Chamwino, Nyembera Moses akizungumza kwenye mafunzo hayo ya Kilimo Bora cha Korosho. Mmoja wa wakulima akizungumza kwenye mafunzo hayo. Meneja wa Bodi ya Korosho Kanda ya Kati na Ma

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI OKTOBA 1,2020

Image
 

WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUACHA UFUGAJI WA MAZOEA

Image
  Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Tz Bwana Imani Sichalwe (aliyevaa koti jeupe) akiwa na wawikilishi wa wafugaji kutoka mikoa mbalimbali waliopatiwa Mafunzo ya ufugaji wa kisasa yaliyofanyika Kwenye ofisi za Uwakala wa Vyuo vya mafunzo ya Mifugo kampasi ya Tengeru Jijini Arusha. Na.Vero Ignatus,Arusha Wafugaji Nchini wametakiwa kuacha Ufugaji wa mazoea na kugeukia Ufugaji wa Kisasa Katika Kipindi hiki cha  ongezeko la Uanzishwaji wa Viwanda vingi vya Nyama Nchini. Akizungumzia wakati wa kufunga mafunzo ya ufugaji wa Kisasa yaliyotolewa kwa Wafugaji wa Mikoa ya Arusha,Dar es salaam,na Manyara yaliyofanyika Kwenye ofisi za Wakala wa vyuo vya mafunzo ya mifugo kampasi ya Tengeru Mkoani Arusha, Kaimu Msajili bodi ya Nyama Tanzania  Imani Sichalwe  amesema mafunzo hayo ni ngao Muhimu sana kwa wafugaji kwakuwa yanamsaidia Kuongeza fursa za biashara ya mifugo jambo litakalosaidia kuongeza thamani ya nyama ndani na nje ya nchi. Kwa Upande wake James Taki akiwa ni Mfugaji kutoka wilaya ya ngoron

HUDUMA YAMAJI YAZIDI KUIMARIKA KATAVI

Image
    Wataalam wa sekta ya maji wakikagua mfumo unaochukua maji kutoa ziwa Tanganyika katika mrdi wa maji wa kijiji cha Karema. Sehemu ya mradi huo imekamilishwa kwa kuwatumia wataalam wa Wizara ya Maji kupitia utaratibu wa force account. 1.    Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (kushoto) akijidhirisha kuhusu upatikanaji wa maji katika kijiji cha Werema, wilayani Tanganyika ambapo wananchi wanapata huduma hiyo katika vizimba 14 vya umma.       Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (kushoto), akimsikiliza Afisa Tarafa wa kijiji cha Karema, wilayani Tanganyika Bw. Mbonimpaye Mtiyonza Nkoronko, anayeelea kuhusu huduma ya maji katika eneo lake la kazi, ambapo huduma hiyo inatolewa kwa saa 24, katika vituo 14 vya wananchi, na baadhi waliounganishiwa katika makazi yao. Huduma ya maji mkoani Katavi inazidi kuimariki baada ya miradi ya maji iliyokuwa ikitekelezwa kukamilika na wananchi kuanza kupata huduma hiyo