Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI SEPTEMBA 20, 2020

Image
 

WAZIRI ZUNGU, RC KUNENGE WASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA PENDEZESHA TANZANIA INAYORATIBIWA NA CRDB

Image
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira *Mhe. Mussa Azzan Zungu* leo amezindua Kampeni ijulikanayo Kama *PENDEZESHA TANZANIA* inayolenga kutunza na kuhifadhi mazingira kwa mustakabali Wa vizazi vya sasa badae kupitia shughuli za upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Nchi. Katika uzinduzi huo *Waziri Zungu* na Mkuu Wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Aboubakar Kunenge* wameshiriki zoezi la usafi na upandaji wa miti kwenye Shule ya Sekondari ya Goba ambapo Mhe. Zungu ameeleza kuwa kampeni hiyo itasaidia pia kukabiliana na athari za Mabadiliko ya tabia nchi Aidha Waziri zungu ameipongeza Bank ya CRDB kwa kuona umuhimu Wa kutunza mazingira ambapo ametoa wito kwa taasisi na wananchi kuanzia ngazi ya familia kupanda miti Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Aboubakar Kunenge* amesema mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha hali ya mazingia inazidi kuwa safi na nzuri ambapo amesema amejidhatiti kuhakikisha miti inayooandwa inatunzwa na kustawi vizuri.  

RAIS MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA BURUNDI NDAYISHIMIYE MKOANI KIGOMA

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na mgeni wake, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kwenye uwanja wa mpira Lake Tanganyika ulioko eneo la Mnarani mkoani Kigoma Septemba 19, 2020. Rais huyo wa Burundi yuko nchini kwa ziara ya siku moja ya kiserikali. Rais Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Septemba 19,2020. Rais Evariste Ndayishimiye akihutubia wananchi  kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli Septemba 19,2020.(PICHA NA IKULU).  

LHRC YAGUSWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA KAMA SEHEMU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA UTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Image
  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Mama wa Huruma kilichopo Madale, Dar es Salaam.  LHRC wamefanya tukio hilo la kiutu Ijumaa, Septemba 11, 2020 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwake (LHRC).  Akizungumza na wanahabari, mwakilishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Naemy Sillayo amesema LHRC wameamua kutembelea kituo cha kulea watoto kama sehemu ya muendelezo wa kupaza sauti kukemea ukiukwaji wa haki za watoto na kuisihi jamii kuongeza ulinzi kwa watoto.  “Kwetu sisi (LHRC) hii si mara ya kwanza kutembelea vituo hivi vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, tunafanya hivi kwa kuwa moja ya kazi yetu kubwa ni kuhamasisha ulinzi wa haki za watoto hapa nchini. Tunaposheherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa LHRC tunaendelea kuonesha kwamba tunaguswa sana na ukiukwaji wa aina yoyote ile wa haki za watoto na pia tunachukua hatua kuhakikisha haki za watoto zinalindwa"

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 19, 2020

Image
 

JPM “AITEKA” KIGOMA, UWANJA WA LAKE TANGANYIKA WAFURIKA, WATAPIKA

Image
NA SAID MWISHEHE, MICHUZI TV-KIGOMA MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali yake imepanga kununua meli mbili ambazo zitafanya kazi katika Ziwa Tanganyika. Miongoni mwa meli hizo mpya, mmoja itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 400 na abiria 600 huku meli nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 4000. Akizungumza leo Septemba 18, 2020, mbele ya maelfu ya wananchi Dk.Magufuli amesema mbali ya kununua meli hizo pia, imepanga kuzifanyia matengenezo meli za MV Liemba ambapo na MV Sangara na kiasi cha Bilioni 16 zitatumika. "Leo tarehe 18.9 andikeni kuwa tunayosema yanatoka moyoni, mimi sitoi ahadi hewa, nataka Kigoma mfanye biashara , tunanunua meli mpya mbili , nimechoka kusikia ajali kwenye ziwa Tanganyika , hivyo tunataka kutengeneza muelekeo mpya wa Kigoma,"amesema Dk.Magufuli. Amesema mpango mwingine ni kujenga ofisi kubwa ya bandari ambayo itahudumia bandari zote zilizopo Ziwa Tangan

WAKILI MKUU WA SERIKALI AWAPONGEZA WAFANYAKAZI KWA MAFANIKIO MAKUBWA YALIYOPATIKANA NDANI YA MUDA MFUPI

Image
NA DENNIS BUYEKWA – MOROGORO SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mh . Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na watumishi wa Umma wakiwemo watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kuiletea maendeleo nchi yetu. Hayo yamezungumzwa mapema leo na Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Gabriel Pascal Malata wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) uliopo mkoani Morogoro. Bw. Malata amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo mwaka 2018, ofisi yake imeendelea kutekeleza vyema majukumu yake ya Uratibu, Usimamizi, Ushauri, na Uendeshaji wa Mashauri yote ya Madai na Usuluhishi yanayofunguliwa dhidi ya Serikali pamoja na Taasisi zake ndani na nje ya nchi. Ameongeza kuwa ili tuweze kufikia malengo ya vipaumbele vikubwa katika nchi yetu ambavyo vimewezesha kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya Uchumi wa kati, kuvutia wawekezaji