Saturday, September 19, 2020

WAZIRI ZUNGU, RC KUNENGE WASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA PENDEZESHA TANZANIA INAYORATIBIWA NA CRDB


Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira *Mhe. Mussa Azzan Zungu* leo amezindua Kampeni ijulikanayo Kama *PENDEZESHA TANZANIA* inayolenga kutunza na kuhifadhi mazingira kwa mustakabali Wa vizazi vya sasa badae kupitia shughuli za upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Nchi.

Katika uzinduzi huo *Waziri Zungu* na Mkuu Wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Aboubakar Kunenge* wameshiriki zoezi la usafi na upandaji wa miti kwenye Shule ya Sekondari ya Goba ambapo Mhe. Zungu ameeleza kuwa kampeni hiyo itasaidia pia kukabiliana na athari za Mabadiliko ya tabia nchi

Aidha Waziri zungu ameipongeza Bank ya CRDB kwa kuona umuhimu Wa kutunza mazingira ambapo ametoa wito kwa taasisi na wananchi kuanzia ngazi ya familia kupanda miti

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Aboubakar Kunenge* amesema mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha hali ya mazingia inazidi kuwa safi na nzuri ambapo amesema amejidhatiti kuhakikisha miti inayooandwa inatunzwa na kustawi vizuri.

 

0 comments:

Post a Comment