RC SHIGELLA ALISHUKURU SHIRIKA LA WORLVISION TANZANIA KWA KUWEKEZA KWENYE MRADI MKUBWA WA MAJI MKINGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua,kutembelea miradi ya maji kujionea namna unavyotekelezwa eneo la Horohoro Mkinga mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwan i na mazingira ya miundombinu pamoja na kuzindua mtambo wa umeme jua uliosimikwa hapo kwa ajili ya kusukuma maji wilayani Mkinga kulia ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari akizungumza wakati wa ziara hiyo Mratibu wa Mradi huo kutoka Shirika la World Vision,Damian Sanka kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela kushoto wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Duga Maforoni wenye thamani ya Sh milioni 471 uliojengwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Japan